ADEM Logo
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA

Tunajenga utamaduni wa kuheshimu haki za binadamu, misingi ya utawala bora na utu wa mtu
ADEM Logo

Idara ya uchunguzi na malalamiko

i) kufanya uchunguzi juu ya mambo yanayohusu uvunjaji wa haki za binadamu na ukiukwaji wa misingi ya utawala bora;

(ii) Kuchukua hatua zipasazo kwa ajili ya kukuza na kuendeleza usuluhishi na suluhu miongoni mwa watu na taasisi mbalimbali wanaofika au kufikishwa mbele ya Tume

(iii) Kuandaa programu za kukuza haki za binadamu na utawala bora kwa watu walio katika nafasi za uongozi katika sekta ya umma na sekta binafsi;

(iv) Kuandaa na kutekeleza mikakati ya  ulinzi na ukuzaji wa haki za binadamu na misingi ya utawala bora;

(v) Kuandaa na kutekeleza programu za kushughulikia haki za makundi maalum ikiwemo watoto, akinamama, wazee na walemavu;

(vi) Kuchunguza mwenendo wa mtu yeyote anayehusika au taasisi yoyote inayohusika na uvunjaji wa haki za binadamu na ukiukwaji wa misingi ya utawala bora katika utekelezaji wa kawaida wa madaraka ya kazi au majukumu yake au utekelezaji unaokiuka madaraka hayo;

(vii) Kutoa mapendekezo kwa Serikali na vyomno vingine vya umma na vya sekta ya binafsi kuhusu haki za binadamu na utawala bora  baada ya kufanya uchunguzi na kubaini uvunjaji wa haki za binadamu au ukiukwaji wa misingi ya utawala bora; na

(viii) Kufuatilia na kuchunguza matukio ya kila siku ya uvunaji wa haki za binadamu na ukiukwaji wa misingi ya utawala bora kutoka vyanzo mbalimbali ikiwemo vyombo vya habari;