ADEM Logo
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA

Tunajenga utamaduni wa kuheshimu haki za binadamu, misingi ya utawala bora na utu wa mtu
ADEM Logo

TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA YASHINDA KESI DHIDI YA TLS

14 Mar, 2026
TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA YASHINDA KESI DHIDI YA TLS

Mahakama Kuu Tanzania kanda ya Dar es Salaam imeitupilia mbali shauri la kikatiba lililofunguliwa na Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) dhidi ya Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB), Inspekta Jenerali wa Polisi na Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Katika shauri hilo TLS ilidai kuwa THBUB ilishidwa kutekeleza jukumu la kulinda haki za binadamu katika kipindi cha amri ya kutotoka nje iliyotolewa na Inspekta Jenerali wa Polisi tarehe 29 Oktoba 2025 na hivyo kuitaka Mahakama kutamka kuwa amri hiyo ilikiuka haki za binadamu.
 
Katika kesi hiyo TLS ilidai kuwa haki za msingi za binadamu, ikiwemo haki ya uhuru wa mtu binafsi, uhuru wa kutembea pamoja na haki ya kuishi zilikiukwa, na kwamba THBUB haikutekeleza ipasavyo wajibu wake wa kulinda na kutetea haki hizo wakati wa utekelezaji wa amri ya kutotoka nje.
 
Aidha, TLS iliomba Mahakama kuunda Tume huru ya uchunguzi yenye wajumbe saba kutoka Tume ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu,Chama cha Mawakili Tanganyika, Chama cha Madaktari, Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa na Jumuia ya Madora  ili kuchunguza hatua zilizochukuliwa na Inspekta Jenerali wa Polisi kuhusu utekelezaji wa amri hiyo.
 
Katika usikilizwaji wa shauri hilo, THBUB iliwakilishwa na Mkurugenzi wa Idara ya Huduma za Kisheria katika Tume Wakili Msomi Bi. Ellen Rwijage, Mkurugenzi Msaidizi Sehemu ya Uendeshaji Mashauri katika Tume Wakili Msomi Bi. Rosemary Shio, Afisa Sheria Daraja la II katika Tume Wakili Msomi Bw. Majid Kangile, Wakili Msomi              Bw. Pontian Kitorombombo na  Wakili Msomi Bw. Joshua Matiko waliowasilisha hoja za Tume katika usikilizwaji wa kesi hiyo wakishirikiana na Mawakili Wasomi kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Awali na kabla ya usikilizwaji wa kesi hiyo, Mawakili Wasomi hao waliwasilisha pingamizi la awali kuhoji mamlaka ya Mahakama katika kutoa nafuu zilizoombwa na TLS walikuwa wakimwakilisha Wakili Msomi Boniface Mwabukusi aliyekuwa Mlalakmikaji kwenye shauri hilo.
 
Upande wa THBUB uliieleza Mahakama kuwa haina mamlaka ya kuunda Tume ya Uchunguzi kama ilivyokuwa ikiombwa na TLS, kwani kwa mujibu wa kifungu cha 3(1) cha Sheria ya Tume ya Uchunguzi mamlaka hayo yapo kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pekee.
 
Baada ya kusikiliza hoja za pande zote, Mahakama ilikubaliana na hoja za THBUB kwamba Mahakama Kuu haina mamlaka ya kuunda Tume ya Uchunguzi kama ilivyokuwa ikiombwa na TLS, kwani mamlaka hayo kisheria yapo kwa Rais pekee.
 
 Aidha, Mahakama ilibainisha kuwa hati ya kiapo iliyowasilishwa kuunga mkono madai hayo ilikuwa na kasoro, ikiwemo kuwepo kwa tarehe zisizolingana kuhusu utolewaji wa amri ya kutotoka nje.
 
Kutokana na kasoro hizo za kisheria, Mahakama iliamua kutupilia mbali shauri hilo kwa kuwa halikuwa na uhalali wa kisheria wa kuendelea kusikilizwa, huku kila upande ukibeba gharama za kesi.
 
Uamuzi huo uliotolewa Machi 11, 2026 na Waheshimiwa Jaji Banzi, Jaji Mtulya na Jaji Mnyukwa unaonesha umuhimu wa kufuata taratibu sahihi za kisheria katika kuwasilisha mashauri mahakaman