07
Sat, Dec
12 New Articles

Top Stories

Grid List

Kama tunavyofahamu kuwa siku ya Jumapili Novemba 24, 2019 Watanzania kote nchini watafanya uchaguzi wa viongozi ngazi ya Serikali za Mitaa. Hatua hiyo ya uchaguzi imetanguliwa na uandikishaji wapiga kura, uteuzi wa wagombea na kampeni za wagombea, hatua ambazo zimetekelezwa kwa mafanikio makubwa.

 

Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) imeridhishwa na idadi ya watu waliojitokeza kujiandikisha kupiga kura. Idadi hiyo imeongezeka ukilinganisha na idadi ya watu waliojiandikisha katika uchaguzi kama huo uliofanyika mwaka 2014.Soma Zaidi

 

Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) imepokea taarifa zinazohusu askari polisi kuwapiga na kudhalilisha watu wenye ulemavu katika tukio lililotokea asubuhi ya Jun 16,2017,Mtaa wa Sokoine Jijini Dares Salaam.Soma zaidi

 

 

Crime affected citizen thoughts

Press Release

Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) imepata taarifa kupitia vyombo vya habari kuhusu uvamizi wa kituo cha Luninga na Radio cha Clouds Media Group, uliofanywa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Paul Makonda, usiku wa tarehe 17, Machi mwaka huu, akiwa na askari wenye silaha.

Hotuba ya Mheshimiwa Bahame Tom Nyanduga, Mwenyekiti wa Tume katika siku ya kupinga mateso na ukatili dhidi ya wazee duniani, tarehe 15 Juni 2017, yaliyofanyika katika ofisi za Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Jengo la Haki, Dar es Salaam. Pakua hotuba kamili

Hotuba ya Mhe. Bahame Tom Nyanduga, Mwenyekiti wa Tume wakati wa hafla ya utoaji tuzo za umahiri wa uandishi wa habari tanzania (EJAT) 2015, ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam, aprili 29, 2016. Pakua hotuba kamili

Hotuba ya mwenyekiti wa Tume Mhe. Bahame T. Nyanduga, katika ufunguzi wa mkutano wa wadau kuhusu mikakati ya kukomesha mauaji na ukatili dhidi ya watu wenye ulemavu wa ngozi , tarehe 18 Machi 2015 katika ofisi za Tume. Pakua hotuba kamili

Jaji Mkuu wa Mahakama Kuu, Zanzibar, Omary Othman Makungu (katika) akiwa katika picha ya pamoja na Mwenyekiti wa THBUB, Jaji Mstaafu Mathew Mwaimu(kulia kwake) na Viongozi wengine wa tume. Mwenyekiti wa tume alimtembelea Jaji Mkuu ofisini kwake Desemba 2, 2019.

News

Jaji Mkuu wa Mahakama Kuu, Visiwani Zanzibar, Omary Othman Makungu amemueleza Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB), Jaji Mstaafu Mathew Mwaimu kuwa wako tayari kushirikiana tume kutatua kero za wananchi zinazohusu upatikanaji wa haki nchini.

Jaji  Makungu alisema hayo alipokutana na Mwenyekiti wa tume ofisini kwake Visiwani Zanzibar Desemba 2, 2019. 

Mwenyekiti wa THBUB Jaji Mstaafu Mathew Mwaimu akiongea katika kikao kilichofanyika Desemba 2, 2019 katika ofisi za Baraza la Wawakilishi. Kulia ni Spika wa Baraza la Wawakilishi Visiwani Zanzibar, Zubeir Ali Maulid.

News

Spika wa Baraza la Wawakilishi Visiwani Zanzibar, Zubeir Ali Maulid amemueleza Jaji Mstaafu Mathew Mwaimu kuwa kazi aliyopewa kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) ni kubwa na ngumu.

Spika Maulid alieleza hayo katika kikao kilichofanyika kwenye  ofisi za Baraza la wawakilishi  mapema leo (Desemba 2, 2019) alipotembelewa na Mwenyekiti huyo.

Mwenyekiti wa (THBUB), Jaji Mstaafu Mathew Mwaimu akiongea na wafanyakazi wa tume pamoja na wageni wengine waliohudhuria hafla fupi.

News

Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB), Jaji Mstaafu Mathew Mwaimu ametembelea ofisi za taasisi hiyo zilizopo visiwani Zanzibar, ikiwa mara yake ya kwanza tangu alipokabidhiwa  dhamana hiyo Novemba 4, 2019.

 MAONI YA WANANCHI KUHUSU WAOMBAJI WANAOITWA KWENYE USAILI KWA AJILI YA NAFASI ZA MWENYEKITI, MAKAMU MWENYEKITI NA MAKAMISHNA WA TUME

Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) ni taasisi huru ya umma na inayojitegemea iliyoanzishwa chini ya Ibara ya 129(1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Sura ya Pili ya Sheria yenye majukumu ya kuhakikisha kuwa haki za binadamu na utawala zinakuzwa, kulindwa na kuheshimiwa  nchini

Kamati ya Uteuzi  inawaalika  raia wa Tanzania wenye sifa zinazotakiwa kuwasilisha maombi kwa nafasi ya Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na Makamishna ili  kujaza nafasi zilizo  wazi katika Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora.Pakua Habari kamili . Read more

 

TUNAPENDA KUWATANGAZIA WADAU NA WATEJA WOTE WA TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA KWAMBA OFISI ZETU ZILIZOPO JENGO LA TANCOT ZIMEHAMIA JENGO LA WIZARA YA KATIBA NA SHERIA MTAA WA MKWEPU. HIVYO HUDUMA ZOTE ZITATOLEWA HUKO KUANZIA TAREHE 01 JANUARI, 2019

UTAWALA

Advertisement