Idara ya Utawala na Rasilimali Watu
i. Kutoa utaalamu na huduma zinazohusiana na masuala ya utawala na usimamizi wa rasilimaliwatu katika Tume
ii.Kutoa ushauri kuhusu masuala ya kiutawala na usimamizi wa rasilimali watu;
iii.Kutoa michango ya kimkakati kuhusu masuala ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu kama vile ajira, upandishaji vyeo , maendeleo ya rasilimali watu na mafunzo, kusimamia taratibu za nidhamu, uhifadhi wa watumishi, motisha, usimamizi wa utendaji kazi na maslahi ya wafanyakazi;
iv. Kufasiri Kanuni za Huduma za Umma, Taratibu za Kudumu (Standing Orders) na sheria nyingine za kazi;