ADEM Logo
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA

Tunajenga utamaduni wa kuheshimu haki za binadamu, misingi ya utawala bora na utu wa mtu
ADEM Logo

ZIARA YA KAMISHNA WA OPERESHENI NA MAFUNZO JESHI LA POLISI, OFISI ZA THBUB MAKAO MAKUU

30 Sep, 2024
ZIARA YA KAMISHNA WA OPERESHENI NA MAFUNZO JESHI LA POLISI, OFISI ZA THBUB MAKAO MAKUU

Leo Septemba 30, 2024 Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) imepokea ugeni wa Kamishina wa Operesheni na Mafunzo kutoka Jeshi la Polisi  Tanzania, CP Awadhi Juma Haji.

Ugeni huo umepokelewa na Makamu Mwenyekiti wa THBUB Mhe. Mohamed Hamis Hamad akiambatana na Makamishina wa THBUB Mhe. Dkt.Thomas Masanja, Mhe. Amina Talib Ali, Mhe Nyanda Shuli na  Mkurugenzi wa malalamiko na Uchunguzi Bi. Suzan Ndeona  pamoja na maafisa wengine wa Tume.

Lengo la ugeni huo ni kuitikia wito wa THBUB wa kuja kuzungumzia tuhuma zilizoripotiwa na vyombo vya habari pamoja na wadau mbalimbali wa demokrasia  dhidi ya askari wa Jeshi la Polisi kukamata, kupiga na kuharibu mali za viongozi na wanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) pamoja na waandishi wa habari.

Ikumbukwe kuwa tuhuma hizo zilitokea tarehe 11 Agosti 2024, ambapo viongozi na wafuasi wa CHADEMA walikuwa wanafanya maandalizi ya maadhimisho yaliyozuiliwa na Jeshi la Polisi ya Siku ya Vijana Duniani tarehe 12 Agosti 2024.

Katika  kikao hicho, Tume ilitumia nafasi hiyo kushauriana na Kamishna Awadhi masuala ya mbalimbali yanayohusu ulinzi wa haki za binadamu katika masuala ya  siasa  na uchaguzi