Waziri wa Katiba na Sheria Mhe.Balozi Pindi azindua kamati ya Kitaifa ya Kusimamia mpango kazi wa uandaaji haki za binadamu na biashara.
Serikali ya Tanzania imedhamiria kukamilisha kutengeneza Mpango Kazi wa Kitaifa wa Masuala ya Haki za Binadamu na Biashara, ambao mchakato wake umeanza kwa kuwashirikisha wadau mbalimbali wa Serikali, Asasi za kiraia na Sekta ya Biashara.
Akizungumza wakati wa kuzindua Kamati ya Kitaifa ya kusimamia Uandaaji wa Mpango Kazi huo mjini Arusha leo, Waziri wa Katiba na Sheria Mheshimiwa Balozi Dkt. Pindi Chana , alisema jitahidi za Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan za kuvutia wawekezaji zinahitaji kutungiwa Sera itakayosmimamia ulinzi wa haki za binadamu katika eneo la biashara.
Balozi Chana alitaja maeneo ambayo uwekezaji wake umekuza uchumi kuwa ni pamoja na sekta za uzalishaji, miundombinu, nishati, mawasiliano ya kidigitali, utalii, uziduaji , usafirishaji na biashara kwa njia ya mtandao.
“Kutokana na juhudi hizo za Serikali,sote tumeshuhudia katika miaka ya hivi karibuni, Tanzania ilifikia hadhi ya uchumi wa kipato cha kati unaohitaji juhudi za pamoja kushughulikia uwajibikaji wa biashara”, alisema Mhe Chanda
Aidha Kutokana na kukua kwa shughuli za uwekezaji zinazoweza kuleta matokeo chanya au hasi kwa haki za binadamu na watu, Serikali inatarajia kuandaa mfumo wa kusimamia masuala ya haki za binadamu na biashara kupitia Mpango Kazi wa Haki za Binadamu na Biashara.
“Ni matarajio yangu kuwa Kamati hii, ninayoizundua leo, na ambayo inajumuisha makundi mbali kutoka Serikalini, Asasi za Kiraia na Sekta ya Biashara, itahakikisha kuwa Mpango Kazi utapambanua na kuelelezea vipaumbele na masuala yatakayoungwa mkono katika utekelezaji wa Wajibu wa Kitaifa, Kimataifa na Kikanda wa masuala ya haki za binadamu na biashara’’.alisema Mhe.Chana
Wakatin huo huo, Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Mheshimiwa Jaji (Mstaafu) Mathew Mwaimu alieleza kuwa uamuzi wa Serikali ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar wa kuanzisha mchakato wa kuandaa Mpango Kazi wa Kitaifa wa Masuala ya Haki za Binadamu na Biashara ni uthibitisho wa nia njema na utashi wa kisiasa wa kutengeneza mazingira wezeshi na mazuri ya kuvutia wawekezaji na kuimarisha shughuli za biashara zinazoheshimu haki za binadamu nchini.
“Nia ya Serikali zetu ni kiashiria tosha cha kuungana na mataifa mengine ya wanachama wa Umoja wa Mataifa kutekeleza Mwongozo wa Kanuni za Umoja wa Mataifa wa Haki za Binadamu na Biashara, yaani, United Nations Guiding Principles on Business and Human Rights (UNGP-BHR), uliopitishwa na Baraza Kuu Umoja wa Mataifa mwaka 2011”.alisema Mheshemiwa Mwaimu
Aidha Mhe. Mwaimu. alisema kuwa Mwongozo huu inaweka wajibu kwa Serikali kulinda haki za binadamu, wajibu kwa sekta ya biashara kuheshimu haki za binadamu na kuweka mikondo ya kupata shufaa (nafuu) kwa waathirika wa uvunjwaji wa haki za binadamu unaotokana na shughuli za biashara.
Kamati hiyo ya Kitaifa itakuwa chini ya uenyekiti wa Dkt Khatib Kazungu, ambaye ni Naibu Katiba Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria. Wajumbe wa Kamati hiyo ni pamoja na : Bw.Omar Haji Gora, Naibu Katibu Mkuu, Afisi ya Rais- Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora Zanzibar;Bwa. Saalhina Mwita Ameir, Naibu Katibu Mkuu-0Afisi ya Makam wa Pili wa Rais Zanzibar; Mheshimiwa Mohamed Khamis Hama, Makam Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Borana Bw.Salhina Mwita Ameir kutoka Afisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar;
Wengine ni Bi. Judith Rushohola, Mkurugenzi ewa Huduma za Kisheria, Ofisi ya Waziri Mkuu-Sera, Bunge na Uratibu; Bi. Nana Rowland Mwanjisi, Mkurugenzi wa Mipango, Utafiti na Sera wa Wizara ya Fedha na Mipango Zanzibar; Bi. Magreth Maganga, Mkurugenzi wa Mtaalam wa Sheria na Uandishi wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania; Bwana Onesmo Olengurumwa, Mkurugenzi wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania. Bi. Jovina Muchunguzi, Mratibu wa Miradi na Afisa Uchunguzi Mkuu kutoka Tume ya Haki za Binadamu ameteuliwa kuwa Katibu wa Kamati hiyo.
Wajumbe hao wameanza mafunzo ya siku mbili ya kupanua elewa wa masuala ya haki za binadamu na biashara, hasa kuhusu hatua za mchakato wa Kutengwneza Mpango Kazi wa Masuala ya Biashara na Haki za Binadamu.