ADEM Logo
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA

Tunajenga utamaduni wa kuheshimu haki za binadamu, misingi ya utawala bora na utu wa mtu
ADEM Logo

WATUMISHU THBUB WAMETAKIWA KUTUMIA MKUTANO WA BARAZA LA WAFANYAKAZI KUJADILI YANAYOLETA TIJA KATIKA KAZI

29 Jan, 2025
WATUMISHU THBUB WAMETAKIWA KUTUMIA MKUTANO WA BARAZA LA WAFANYAKAZI KUJADILI YANAYOLETA TIJA KATIKA KAZI

Watumishi wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) wametakiwa kutumia mikutano ya Baraza la wafanyakazi kujadili mambo yanayoleta tija katika kuongeza ufanisi wa kazi. 


Kauli hiyo imetolewa Leo Januari 28, 2025 na Afisa Elimu Kazi Kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu Bi. Tulia Msemwa wakati wa kikao cha kuchagua Wajumbe Wapya  wa Baraza la wafanyakazi la THBUB baada ya wajumbe waliokuwepo kumaliza muda wao.


Bi. Msemwa amesema kuwa Baraza la Wafanyakazi  ni sehemu sahihi ya kujadili, kushauri na kutoa mapendekezo juu ya njia sahihi ya kuongeza ufanisi wa kazi  utakaosaidia kuweka mazingira mazuri kwa Wafanyakazi na Taasisi kwa ujumla.

“hivyo niwaombe wajumbe mtakaochaguliwa hakikisheni mnatumia vyema nafasi hiyo kwa kujadili yale yatakayokuwa na tija kwa watumishi wote.”amesema Bi.Msemwa

Naye, Mwenyekiti wa kikao hicho Bw. Fraksed Mushi ambaye pia ni Mkurugenzi Msaidizi wa Rasilimali Watu THBUB, amesema kuwa kila mjumbe aliyechaguliwa  anawajibu wa kutumia nafasi hiyo kushauri na kutoa maoni yatakayo saidia kujenga Mazingira bora kwa wafanyakazi katika  utekelezaji wa majukumu ya kila siku.

“Tumieni Baraza hili katika kujadili mambo muhimu na kutoa mapendekezo sahihi juu ya kuboresha mazingira ya kazi, Idara na Vitengo ili kuongeza tija na ufanisi katika kutekeleza majukumu ya kuendeleza taasisi” amesema Bw. Mushi.

Jumla ya wajumbe tisa (9) walichaguliwa katika kikao hicho ambapo watatumikia nafasi hizo kwa muda wa miaka mitatu.