WATUMISHI THBUB MAKAO MAKUU WASHIRIKI MEI MOSI KITAIFA

Watumishi Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Ofisi ya Makao Makuu wameungana na Watumishi wengine kushiriki Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Wafanyakazi Duniani,ambayo yamefanyika Viwanja vya Bombadia Singida.
Mgeni rasmi katika Maadhimisho hayo yaliyo hudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali pamoja na vyama vya wafanyakazi alikuwa ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan.
Rais Dkt.Samia amesema kuwa katika kuzidi kuleta ustawi kwa wafanyakazi nchini,serikali imefanya maamuzi ya kupandisha kima cha chini cha mishahara kwa watumishi wa umma kwa asilimmia 35.1 .
‘’Serikali kupandisha mishahara imewezeshwa na kasi ya ukuaji Uchumi kupanda hadi kufikia 5.5. asilimia kwa mwaka,hali iliyochangiwa na wafanyakazi kujituma na kufanya kazi kwa bidii’’amesema Mhe.Dkt Samia.
Kwa upande wa wafanyakazi wa sekta binafsi,Rais Dkt. Samia amesema kuwa Bodi ya kima cha chini cha Mshahara inaendelea na tathmini kwa lengo la kuboresha viwango vya mishahara kwa sekta binafsi
Pia,Rais Dkt.Samia amebainisha kuwa serikali itaendelea kushirikiana na wafanyakazi kuzifanyia kazi changamoto zinazowakabili
Maadhimisho ya siku ya wafanyakazi imebebwa na kauli mbiu isemayo”Uchaguzi Mkuu 2025,utuletee Viongozi wanaojali Haki na Maslahi ya Wafanyakazi ,Sote Tushiriki’