WANANCHI WAIOMBA THBUB KUENDELEA KUTOA ELIMU YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA MAENEO YA VIJIJI.
03 Jul, 2025

Wananchi wameiomba Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Kutoa elimu ya haki za binadamu na utawala bora katika maeneo ya vijijini ili waweze kujua haki zao.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti Wananchi hao wamesema kuwa watu wengi udhulumiwa haki zao kutokana kuwa hawajui mahala sahihi kupata haki zao pindiinapotokea imekiukwa.
"Unakutwa mtu amekamatwa bila kufuata utaratibu tunaona sawa kwakua hatujui"amesema
Pia wananchi hao wameishukuru kwakufika Maonesho ya Kimataifa ya Biashara ya Sabasaba ambapo imekua fursa kupata elimu hiyo