ADEM Logo
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA

Tunajenga utamaduni wa kuheshimu haki za binadamu, misingi ya utawala bora na utu wa mtu
ADEM Logo

WANANCHI MKOANI KAGERA WATAKIWA KUTOSITA KUPELEKA MALALAMIKO YAO YANAYOHUSU UVUNJIFU WA HAKI ZA BINADAMU

21 Apr, 2025
WANANCHI MKOANI KAGERA WATAKIWA KUTOSITA KUPELEKA MALALAMIKO YAO YANAYOHUSU UVUNJIFU WA HAKI ZA BINADAMU

Wananchi Mkoani Kagera watakiwa kutosita kupeleka malalamiko yao yanayohusu uvunjifu wa haki za binadamu.

Hayo yameelezwa na  Mfawidhi wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora  Ofisi ya Mwanza. Bw.Gordian Binamungu wakati akizungumza na wateja waliofika katika banda la THBUB kupitia Kampeni ya Msaada wa Kisheria wa Mama Samia( Mama Samia Legal Aid Campaign) ambayo yameanza Aprili 14 hadi 23 2025 katika uwanja wa general Mayunga,Bukoba Mjini


Bw.Binamungu amesema kuwa THBUB  imepewa Mamlaka ya kusimamia na kulinda haki za binadamu nchini

“Hivyo wananchi mkoani kagera na maeneo jirani msisite kufika kupata elimu pamoja nakuwasilisha malalamiko yenu kama yapo”amesema Bw. Binamungu.

Aidha Bw.Binamungu ameongeza kuwa mbali na utoaji wa elimu na upokeaji wa malalamiko ,THBUB inafanya usuluhu wa masuala mbalimbali ili kuepusha uvinjivu haki za binadamu 

Sanjali na hayo Bw.Binamungu amebainisha malalamiko  yaliyowasilishwa tangia kuanza kwa huduma hiyo mkoani hapo ni masuala ya ardhi ikiwemo migogoro ya mipaka ,eneo moja kuuzwa mara mbili,ndoa  na Mirathi