ADEM Logo
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA

Tunajenga utamaduni wa kuheshimu haki za binadamu, misingi ya utawala bora na utu wa mtu
ADEM Logo

Wanafunzi zingatieni sheria na taratibu za shule

21 Jan, 2025
Wanafunzi zingatieni sheria na taratibu za shule

Wanafunzi watakiwa kuzingatia Sheria na taratibu zilizowekwa shuleni ili kupata haki zao na kutimiza wajibu wao kama ilivyoanishwa katika Katiba ya Jamhuri  ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977. Na Sheria ya Mtoto ya Mwaka 2009.

Hayo yamesemwa na Makamu Mwenyekiti  wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THUBU)  wakati wa kutoa elimu ya haki za Mtoto na Ukatili Dhidi ya Watoto katika Shule ya Sekondari  ya Margareth sitta iliyopo wilaya ya Urambo Mkoani Tabora Januari 17, 2025.

Mhe. Mohamed alisema kuwa kutokana na uendelea kwa utandawazi kumekuwa na mwenendo mbaya wa mmomonyoko wa maadili kwa Wanafunzi hali ambayo husababisha kuvunjwa kwa haki zao za msingi kama vile haki ya kupata elimu.

"Wanafunzi wanaingia katika makundi yasiyofaa matokeo yake wanapata mimba na kusababisha kuacha shule" alisema Mhe. Mohamed

Kwa upande wake Veronica Goodluck, Askari Polisi kutoka Dawati la Jinsia na Watoto katika Kituo cha (W) Urambo alitoa wito kwa Wanafunzi hao kueza  kusoma kwa bidii ili waweze kutimiza  malengo yao.

"Yote yanaezekana  kwakujiepusha kuingia katika makundi yasiyofaa" alisema Bi. Veronica

Naye, Mwanafunzi wa Kidato cha Tatu anayeitwa Mbombilie Elias Shiloti ameishukuru THBUB  kwakutoa elimu kwa wanafunzi hao kwani kufanya hivo imeweza kusaidia Wanafunzi hao kuweza kutambua haki na wajibu