ADEM Logo
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA

Tunajenga utamaduni wa kuheshimu haki za binadamu, misingi ya utawala bora na utu wa mtu
ADEM Logo

Wanafunzi shule za Sekondari wapatiwa ya Elimu ya haki za binadamu na utawala bora kupitia mdahalo

16 Oct, 2024
Wanafunzi shule  za Sekondari wapatiwa  ya Elimu ya haki za binadamu na  utawala bora  kupitia mdahalo

Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) imeendelea kutoa elimu kuhusiana na masuala ya haki za binadamu na utawala bora kwa wanafunzi kutoka Shule mbalimbali za Sekondari zilizopo katika Jiji la Dodoma kupitia Midahalo.

Katika mwendelezo huo leo Oktoba 15, 2024 THBUB imeendesha mdahalo wa awamu ya tatu (3) ulioshirikisha wanafunzi wa shule 10 za Sekondari (O-level) uliofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Shule ya Dodoma sekondari.

Akizungumza katika Mdahalo huo Bw. Said R. Zuberi, Afisa Uchunguzi Mkuu kutoka THBUB amesema kuwa kuna uhusiano wa moja kwa moja kati ya matumizi ya dawa za kulevya, rushwa, uvunjwaji wa haki za binadamu na ukiukwaji wa misingi ya utawala bora na maambukizi ya Virusi vya Ukimwi,

Hivyo amewaasa wanafunzi kujiepusha na matumizi ya Dawa za Kulevya na vitendo vya Rushwa kwani vitendo hivyo vinachangia kwa kiasi kikubwa uvunjwaji wa haki za binadamu na ukiukwaji wa misingi ya utawala bora katika jamii.

"Matumizi ya sindano katika matumizi ya dawa za kulevya, rushwa ya ngono na matukio ya ukatili kama vile ubakaji, ulawiti na ukeketaji yanasababisha maambukizi ya Virusi vya Ukimwi,

"Dawa za kulevya na Rushwa ni chanzo cha kuleta athari kubwa zinazosababisha uvunjwaji ya haki za binadamu na ukiukwaji wa misingi ya utawala bora katika jamii kwani mtu yoyote anaepokea au kutoa Rushwa moja kwa moja anakuwa anakiuka misingi ya utawala bora kama vile uwazi, uwajibikaji, uadilifu, usawa, utawala wa sheria, ufanisi na tija,"Amesema Bw. Said.

Kwa upande wa wanafunzi walioshiriki mdahalo huo Mwanafunzi Grace Charles kutoka shule ya Sekondari ya Itega, ameshukuru uwepo wa midahalo hiyo na kuomba uongozi wa THBUB Kufanya midahalo hii katika mikoa Mbalimbali hapa nchini ili kuwafikia vijana wengi zaidi.

Zaidi ya Shule 10 zimeshiriki mdahalo huo ikiwa ni pamoja na shule ya Makole Sekondari, St.Gaspa Sekondari, Viwandani Sekondari, Ihumwa Sekondari, Itenga sekondari, Umonga Sekondari, Chihanga, Kizota Sekondari Nara, Makole Sekondari na Mihuji Sekondari. 

Shule zilizo shinda na kuingia Fainali ni pamoja na Shule ya Viwandani Sekondari, Chihanga Sekondari, Umonga Sekondari, Mihuji Sekondari, Kizota na Makole Sekondari.

THBUB imekuwa ikiandaa midahalo hii kupitia Klabu za Haki za Binadamu katika Shule za Msingi, Shule za Sekondari na Vyuo kwa miaka mitatu mfululizo,Midahalo hii inasaidia kuongeza uelewa kwa wananfunzi kuhusiana na masuala ya haki za binadamu na utawala bora.