Wakazi wa Mwanza waaswa kutembelea Banda la THBUB kujipatia elimu ya haki za binadamu na utawala bora

Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza Bw. Balandya Mayuganya baaada ya kutembelea banda la Ofisi za Tume za Haki za Binadamu na Utawala Bora na kujipatia elimu kuhusu haki za binadamu na misingi ya utawala bora, amewataka wakazi wa mwanza na viunga vyake kufika kwenye banda hilo ili waweze kupata elimu hiyo na pia kuwasilisha malalamiko yao yanayohusu uvunjwaji wa haki za binadamu na misingi ya utawala bora.
Wito huo ameutoa Januari 25, 2025 wakati alipotembelea banda la THBUB baada ya uzinduzi wa Maonesho ya Wiki ya Sheria yanayoendelea katika Viwanja vya Nyamagana Mjini Mwanza.
Elimu hiyo inatolewa na Watumishi wa Ofisi ya Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora ,Tawi la Mwanza wakiongozwa na Mfawidhi Bw. Goldian Binamungu ikiwa na lengo la kuwaelimisha wananchi juu ya haki zao na misingi ya utawala bora.
Maonesho ya Wiki ya Sheria ya wiki ya sheria yamezinduliwa Januari 25, 2025 na yatatamatika Februari 1, 2025.