WAILES SEKONDARI KUWA MABALOZI WA HAKI ZA BINADAMU

Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) yawataka Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Wailes kuwa Mabalozi wa kueneza haki za binadamu katika jamii zao.
Wito huo umetolewa na Bw. Paul Sulle, Afisa Uchunguzi Mkuu Msaidizi kutoka THBUB wakati akitoa elimu kuhusiana na haki za binadamu na misingi ya utawala bora shuleni hapo, Julai 11, 2025 Jijini Dar es salaam.
Aidha, Bw. Sulle ametoa elimu kwa wanafunzi hao namna ya kupinga vitendo vya ukatili na kwamba ni muhimu kutoa taarifa ya vitendo hivyo pindi vinapotokea katika jamii zetu.
Naye Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo Mwl. Daudi Kassenga ameishukuru THBUB kwa jitihada wanazozifanya za kuhakikisha elimu ya haki za binadamu inawafikia wananchi na kwamba shule yake imepata bahati kubwa kupata elimu hiyo na wataendelea kusimamia haki za Binadamu na misingi ya utawala bora.