Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) yaendelea kutoa Elimu kwa Jeshi la Askari Mageleza na Jeshi la Polisi Singida
                            
                                 23 Jan, 2025
                            
                                
                            
                                Leo Januari 21, 2025 Ujumbe wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) umeendelea kutoa elimu kuhusu haki za binadamu na misingi ya utawala bora kwa Askari wa Jeshi la Polisi na Askari wa Jeshi la Magereza katika Gereza la Singida na Kituo cha Polisi Singida.
Ujumbe wa THBUB uliongozwa na Makamu Mwenyekiti Mhe. Mohamed Khamis Hamad ambapo ameeleza kuwa lengo la ziara hiyo ni kutoa elimu kwa askari hao pamoja na kuangalia uzingatiwaji wa hali ya haki za binadamu kwa watu waliozuliwa katika maeneo hayo.

