ADEM Logo
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA

Tunajenga utamaduni wa kuheshimu haki za binadamu, misingi ya utawala bora na utu wa mtu
ADEM Logo

TIMU YA HAKI KAMBA  YAIBUKA NA USHINDI.

16 Sep, 2025
TIMU YA HAKI KAMBA  YAIBUKA NA USHINDI.

 

Timu ya Wanaume ya kuvuta Kamba ya Haki Sports imeibuka na Ushindi dhidi ya RAS Pwani katika Michuano ya Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali Tanzania (SHIMIWI). Mchezo huo ulichezwa katika Viwanja vya Furahisha Jijini Mwanza mapema leo Septemba 1, 2025.

Akizungumza  mara baada ya mchezo huo,  Kapteni wa Timu ya Kamba Bw. Kilua Mtae ameeleza kuwa, Timu hiyo imejipanga vizuri katika michezo yote  iliyopangwa.

Aidha, Bw. Mtae amewapongeza wachezaji wote kwa  kuwa makini pamoja na kuzingatia sheria zote zinazohusu mchezo huo wa kamba. "Hongereni sana" amesema

Katika Mchezo wa Kamba Wanaume Timu ya Haki imepangwa katika kundi H na kesho inatarajiwa kucheza na Maliasili.

Timu ya kuvuta Haki Sport ni  miongoni  mwa timu kutoka THBUB  ambazo zinazoshiriki  Michezo  ya Kamba Michezo mingine ambayo THBUB inashiriki ni pamoja  na Riadha