ADEM Logo
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA

Tunajenga utamaduni wa kuheshimu haki za binadamu, misingi ya utawala bora na utu wa mtu
ADEM Logo

THBUB YAHAMASISHWA KUWA NA MALENGO YANAYO AKISI DIRA YA MAENDELEO YA 2050

16 Sep, 2025
THBUB YAHAMASISHWA KUWA NA MALENGO YANAYO AKISI DIRA YA MAENDELEO YA 2050

 

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria,  Bw. Franklin Rwezimula ameitaka Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, (THBUB) kuwa na mchango katika kufikia malengo ya Dira ya Maendeleo ya Taifa ya 2050 ambayo imejengwa juu ya misingi ya utawala bora, utawala wa sheria na haki za binadamu. 

 Bw. Rwezimula ameyasema hayo leo  Septemba 23, 2025 wakati akifungua kikao cha ndani “retreat” cha Tume na Menejmenti ya THBUB kilichofanyika katika hoteli ya Edema Mkoani Morogoro. Kikao hicho kimelenga kuboreshaji  taswira, kuimarisha nafasi na kuongeza ufanisi wa THBUB katika kutekeleza majukumu yake.


 Bw, Rwezimula amesema Serikali, inathamini  mchango wa  THBUB katika kuhifahi haki za binadamu na misingi ya utawala bora ambayo ndio ni miongoni mwa  misingi ya  Dira ya Maendeleo ya nchi ya 2050.

“Msingi Mkuu wa Dira ya 2050 ni utawala bora, amani, usalama na utulivu” Amesema Bw. Rwezamula

Bw. Rwezamula amesema dira ya 2050 inatambua kwamba Tanzania imepiga hatua kubwa katika kuboresha demokrasia na utawala bora lakini bado inakabaliana na changamoto kadhaa za kiutawala. 

Hivyo amewataka Makamishna pamoja na menejimenti ya THBUB kutumia  kikao hicho cha ndani  katika kujadiliana namna nzuri ya  kuimarisha taasisi ili iwe sehemu ya kuchangia katika kutekeleza Dira ya Maendeleo ya 2050. 

Akielezea kuhusu matarajio ya Serikali, Bw. Rwezamula amesema Serikali na wananchi wana matarajio makubwa kutoka kwa THBUB

Naye Mwenyekiti wa  THBUB, Mhe. Mathew Mwaimu Jaji(Mst), akitoa shukrani kwa niaba ya THBUB ameishukuru Wizara  ya Katiba na Sheria kwa mchango mkubwa inaoendelea kuutoa kwa THBUB kwa namna Wizara inavyoiangali kwa jicho la kipekee. 

Mhe. Jaji ( Mst) Mwaimu amesema baada ya  kikao hicho cha ndani, THBUB inatarajia kuwa na maazimio ya pamoja ya utekelezaji wa majukumu ya  ili kuhakikisha THBUB mpya inazaliwa. 
Aidha, Mhe. Jaji ( Mst) Mwaimu amesema THBUB ipo tayari kuendelea kushirikiana na Wizara katika nyanja zote za masuala ya Haki za Binadamu na Utawala Bora katika kufikia malengo ya Dira ya Taifa ya 2050.