ADEM Logo
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA

Tunajenga utamaduni wa kuheshimu haki za binadamu, misingi ya utawala bora na utu wa mtu
ADEM Logo

THBUB yawaleta Wadau pamoja kujadili Haki za Binadamu

18 Dec, 2023
THBUB yawaleta Wadau pamoja kujadili Haki za Binadamu

Katika kuadhimisha Miaka 75 ya Tamko la Ulimwengu la Haki za Binadamu,Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Mhe.Mathew Mwaimu (JajiMstaafu) amesema kuwa Tanzania ni miongoni mwa nchi zinazotoa haki za binadamu kwakuridhia mikataba ya kimataifa na kikanda pamoja na kutunga sera mbalimbali na sheria ili kusaidia jamii.

 Hayo amesema  Desemba 14,2023 Jiji Dar es Salam,wakati wa  Kongamano la Maadhisho ya Miaka 75 ya Haki za Binadamu ikiwa ni pamoja na kujadili ,kufanya tathimini ya kutambua mfanikio yaliyopatikana  tangu kutoka kwa azimio hilo.

Aidha  Mhe.Mwaimu, alieleza kuwa Tume, kwa kushiri*-+9kiana na wadau wengine iliandaa shughuli mbalimbali zilizotekelezwa kuanzia Mwezi Januari Mwaka huu zikiwemo: Mafunzo kwa Viongozi na Walezi wa Klabu za Haki za Binadamu kutoka vyuoni;Kufanya maonesho ya kulienzi Tamko la Haki za Binadamukupitia Mabanda ya Maonesho yaliyofanyika jijini Dodoma  kwa siku tano, Kutembelea Magereza na Vituo vya Kulelea Watoto, kutoa elimu kupitia vipindi vya redio, Kutembelea wagonjwa hospitalini na kuwapa misaada ya kiutu na kushiriki katika kongamano la maadhimisho ya Miaka 75 ya Tamko la Ulimwengu la Haki za Binadamu katika Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustinelililoandaliwa na Klabu ya Haki za Binadamu ya Chuo hicho.

kama Tume, ambayo ni Taasisi ya umma tunatambua mchango wa Wadau wote wa haki za binadamu hususan Asasi za Kiraia, watetezi wa haki za binadamu, wanazuoni na wanataaluma, vyombo vya habari na wanafunzi (Vijana) katika kulinda, kukuza na kuimarisha haki za binadamu nchini.

‘ Ni wazi kuwa kongamano hili katika kuadhimisha miaka 75 ya Tamko la Haki za Binadamu, ni moja ya njia muafaka ya kukusanya na kuyaweka pamoja mawazo ya wadau wote ambayo yatasaidia katika kuboresha mtazamo wetu kuhusu haki za binadamu na kutufanya tuendelee kuwa mstari wa mbele katika kutetea na kulinda haki za binadamu hapa Tanzania’.amesema Mhe.Mwaimu

Mhe.Mwaimu alitoa wito kwa washiriki kutoa mawazo na maoni yao juu ya namna ya kuboresha hali ya haki za binadamu nchini.

‘Nina fahamu kuwa nyote mnaoshiriki mafunzo haya mnawakilisha makundi tofauti.Ninaamini elimu tutakayoipata katika Kongamano hili itakuwa chachu ya kulienzi Tamko la Haki za

Binadamu Ulimwenguni kwa kuwa elimisha Watanzania wenzetu katika maeneo tunayotoka na kwa jamii kwa ujumla kwa mustakabali wa nchi yetu kwa kuzingatia Tamko hilo”.amesema Mhe.Mwaimu

Kwahatua nyingine Mhe.Mwaimu alitaja changamoto zilizopelekea kutolewa kwa Tamko la Haki za Binadamu Ulimwenguni ni kuwepo kwa pamoja na; madhara ya mabadiliko ya tabia nchi, umasikini, ujinga na maradhi, kukosekana kwa huduma bora ya Afya, ubaguzi na kutokuwepo kwau sawa, kuwepo kwa baadhi ya vifungu vya sheria zinazokandamiza uhuru wakujieleza, Uharibifu wa Mazingira, kuongezekak wa  idadi ya watu, mapinduzi ya teknolojia na ukatili wa mitandaoni, kuongezekakwaMajangaya Asili, vita,uelewa mdogo wa haki za binadamu miongoni mwa jamii zetu, kuendelea kuwepo wa mila na desturi kandamizi,vitendo vya ukatili wa kijinsia na mmomonyoko wa maadili katika jamii.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji Kituo cha Sheria Haki za Binadamu,Wakili Anna Henga ametoa  wito kwa Vijana kushiriki kikamilifu katika michakato ya Kitaifa hasa katika kupambania haki za binadamu ili kuweka uwiano saw kwani vijana ni kundi lenye nguvu.

Aidha  Wakili Anna ameeleza kuwa vijana wanatakiwa kuwa na utaratibu wa kupitia sheria zile zilizotungwa zamani ili ziundwe upywa kwa sheria hubadilika kulingana  na wakati ili haki itende.

“Sheria zinabadirika badirika,kuna sheria ilikuwepo mwaka 1971 mtoto wa kike wa miaka 13 alikua anaweza kuolewa ila leo haiwezekani,maana bado yuko shuleni,sheria nyingi zimepitiwa na wakati kwakweli hivyo tunapaswa kuzifanyia marejro”.alisema Wakili Anna