THBUB YATEMBELEA KITUO CHA POLISI CHA KATI MKOANI IRINGA

Katika utekelezaji wa Majukumu yake ya Kikatiba na Kisheria, ujumbe wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) ukiongozwa na Kamishna Mhe. Dkt. Thomas Masanja umetembelea Kituo cha Polisi cha Kati Mkoa wa Iringa, Februari 21, 2025.
THBUB umetembelea Kituo hicho cha Polisi kwa na kukagua watu waliozuiliwa kituoni hapo kwa lengo la kutathmini haki za watu hao ili kuweza kubaini changamoto wanazokutana nazo na kuzipeleka katika Mamlaka husika ili kuzipatia ufumbuzi.
Aidha, wakiwa kituoni hapo THBUB ilipata nafasi ya kufika katika Dawati la Jinsia na Watoto lililopo kituoni hapo kwa lengo la kukagua na kujua aina ya malalamiko yanayopokelewa katika dawati hilo na pia kujua ni hatua gani wamezichukua baada ya kupokea malalamiko hayo, pia kuzifahamu changamoto wanazokutana nazo katika kushughulikia malalamiko hayo.
THBUB bado ipo Mkoani Iringa ikiendelea na ziara yake ya kutoa elimu kwa Wananchi na Wanafunzi wa Sekondari na Vyuoni, pamoja na kutembelea Magereza na maeneo mengine wanakozuiliwa watu.