THBUB YATEMBELEA GEREZA LA WILAYA KIBONDO
23 Feb, 2025

Ujumbe wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) ukiongozwa na Kamishna Amina Talib Ali ametembelea Gereza la Nyamisivyi Wilayani Kibondo Mkoa wa Kigoma ambapo amekagua na kusikiliza kusikiliza changamoto mbali mbali zinazowakabili watu wanaozuiliwa katika Gereza hilo Februari 20, 2025.
Mhe. Amina amepongeza Maafisa na Askali wa Jeshi la Magereza Wilaya ya Kibondo kwa kazi nzuri wanayofanya ya kuwarekebisha wafungwa na kuwafanya raia wema pindi wanapotoka Magerezani.