ADEM Logo
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA

Tunajenga utamaduni wa kuheshimu haki za binadamu, misingi ya utawala bora na utu wa mtu
ADEM Logo

THBUB YATEMBELEA GEREZA IRINGA 

23 Feb, 2025
THBUB YATEMBELEA GEREZA IRINGA 

Ujumbe wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) ukiongozwa na Kamishna Mhe.Dkt. Thomas Masanja umetembelea gereza la mkoa wa Iringa kwa lengo la kukagua na kuangalia huduma zinazotolewa kwa wafungwa na mahabusu gerezani hapo, Februari 19, 2025.

Baada ya kukamilisha ukaguzi huo Dkt. Masanja alipata nafasi ya kuongea na wafungwa na maabusu wote ambapo waliweza kutoa changamoto mbalimbali zinazowakabili ambazo zinahohusiana na masuala ya Kisheria.

Dkt. Masanja aliwaahidi wafungwa hao kuwa THBUB itafuatilia changamoto hizo na kuzipatia ufumbuzi.

THBUB ipo mkoani Iringa kutekeleza baadhi ya majukumu yake ambayo ni kutoa elimu na kutembea magereza za mkoa huo.