ADEM Logo
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA

Tunajenga utamaduni wa kuheshimu haki za binadamu, misingi ya utawala bora na utu wa mtu
ADEM Logo

THBUB YAITAKA SERIKALI NA WAAJIRI NCHINI KUENDELEA KUWEKA MAZINGIRA BORA YA KAZI

14 May, 2025
THBUB YAITAKA SERIKALI NA WAAJIRI NCHINI KUENDELEA KUWEKA MAZINGIRA BORA YA KAZI


Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) imeitaka serikali na waajiri wote nchini kuendelea kuweka mazingira bora ya kazi na kusimamia maslahi ya wafanyakazi kwa mjibu wa katiba na sheria za Ajira ili kujenga mazingira rafiki kwa wafanyakazi kufurahia haki zao za kufanyakazi ili kuleta tija na ufanisi katika utendaji wao.
Rai hiyo imetolewa leo Aprili 30,2025 jijini Dodoma na Mwenyekiti wa tume hiyo Jaji mstaafu Mhe.Mathew Mwaimu wakati akitoa Tamko la Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora katika kuelekea maadhimisho ya siku ya wafanyakazi Duniani Mei 1,2025.
Mwaimu amesema maadhimisho hayo yanalenga katika kutambua mchango wa wafanyakazi duniani kote katika kuleta maendeleo ya kiuchumi na kijamii.

Mhe. Mwaimu amesema Maadhimisho haya yanalenga katika kutambua mchango wa wafanyakazi Duniani kote katika kuleta maendeleo ya kiuchumi na kijamii.
“Nitoe rai kwa serikali na waajiri wote nchini kuendelea kuweka mazingira bora ya kazi na kusimamia vyema maslahi ya wafanya kazi kwa mjibu wa katiba na sheria za Ajira ilikujenga mazingira rafiki kwa wafanyakazi kufurahia haki yao ya kufanya kazi na pia kuleta tija na ufanisi katika utendaji,”amesema.

Maadhimisho haya  ya Mei mosi mwaka 2025 yanaenda sambamba na kaulimbiu isemayo “Uchaguzi mkuu 2025 utuletee viongozi wanaojali Haki na maslahi ya wafanyakazi,sote tushiriki”ambapo Mhe.Mwaimu amesema kaulimbiu hiyo inawahamasisha wafanyakazi kujitokeza kushiriki uchaguzi huo ili kuhakikisha kwamba pamoja na wananchi wengine wanashiriki kikamilifu kuwachagua viongozi wenye kusimamia na kulinda haki za binadamu.

Ameongeza kuwa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) inawakumbusha wafanyakazi kuwa upatikanaji wa viongozi waadilifu utapunguza malalamiko ya wafanyakazi hususani katika masuala yanayohusu maslahi yao binafsi.
“Maadhimisho ya siku ya wafanyakazi mwaka 2025 nchini yanaongozwa na kaulimbiu isemayo uchaguzi mkuu 2025 utuletee viongozi wanaojaki haki na maslahi ya wafanyakazi,sote tushiriki kaulimbiu hii inawahamasisha wafanyakazi kujitokeza kushiriki katika uchaguzi mkuu utakao fanyika mwaka huu 2025,”amesema.

Vile vile amesema Tume hiyo inatambua na kupongeza juhudi za serikali ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania katika kuhakikisha nchi inapata viongozi waadilifu,wasiyo na ubaguzi,wenye uzalendo,wanaozingatia haki za Binadamu na misingi ya utawala bora katika utekelezaji wa majukumu yao ili.kuendelea kujenga Taifa lenye amani na utulivu.