ADEM Logo
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA

Tunajenga utamaduni wa kuheshimu haki za binadamu, misingi ya utawala bora na utu wa mtu
ADEM Logo

THBUB YAFANYA UKAGUZI KIWANDA CHA KEDS TANZANIA COMPANY LTD KUJIRIDHISHA NA UZINGATIWAJI WA HAKI ZA BINADAMU

14 Mar, 2025
THBUB YAFANYA UKAGUZI KIWANDA CHA KEDS TANZANIA COMPANY LTD KUJIRIDHISHA NA UZINGATIWAJI WA HAKI ZA BINADAMU

Katika utekelezaji wa majukumu yake ya Kikatiba na Sheria, Ujumbe wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) ukiongozwa na Kamishna Mhe. Nyanda Shuli umetembelea kiwanda cha KEDS TANZANIA COMPANY LYD na kufanya mazungumzo na baadhi ya Wafanyakazi wa kiwanda hicho kilichopo Wilaya ya Kibaha Mji Mkoani Pwani, Machi 12, 2025.

Mazungumzo hayo yalifanyika mara baada ya THBUB kukagua maeneo yote ya kiwanda pamoja na kufanya mazungumzo na Menejimenti ya kiwanda hicho.

Lengo la mazungumzo hayo na ukaguzi ni kuangalia uzingatiwaji wa haki za binadamu na misingi ya utawala bora, kuangalia usalama na mazingira ya kazi na uzingatiwaji wa viwango vya ajira.

Aidha, katika zoezi hilo THBUB imeambatana na taasisi zinazosimamia mazingira, usalama na afya mahala pa kazi ambazo ni Occupational Safety and Health Administration (OSHA), National Environmental Management Council (NEMC)na  Maafisa kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani ambao ni Afisa biashara, Afisa Kazi na Afisa Maendeleo ya jamii kwa lengo la kuleta ufanisi katika ziara hiyo.

THBUB itaendelea na ziara yake katika viwanda vya CPL (TANZANIA) GRAIN PROCESSING AND STORAGE, MAISHA PLASTIC TANZANIA pamoja na METL.