ADEM Logo
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA

Tunajenga utamaduni wa kuheshimu haki za binadamu, misingi ya utawala bora na utu wa mtu
ADEM Logo

THBUB yaapisha Maafisa wapya

24 Jan, 2025
THBUB yaapisha Maafisa wapya

KAMISHNA wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Ofisi ya Zanzibar, Khatib M. Mwinyichande leo tarehe 24 Januari, 2025 amewaapisha Maofisa watatu wa Tume hiyo ofisini kwake Mbweni Wilaya ya Magharibi B, Mkoa wa Mjini Magharibi

Walioapishwa ni Moh'd Suleiman Ali, Afisa Tehema THBUB Pemba, Ismail Mussa Afisa Uchunguzi, Pemba na Muhammed Masoud Said, Afisa Sheria THBUB, Pemba.

Uapisho huo  umeshuhudiwa na  Naibu Katibu Mtendaji THBUB, Juma Msafiri  Karibona na Afisa Mfawidhi Saada A. Masoud. 

Wakati huo huo Kamishna Mwinyichande alikuwa na mkutano wa pamoja na maafisa wote wa THBUB, Zanzibar kwa lengo la kuwapa nasaha na kuwakaribisha kwenye Tume hiyo.

Aidha, Naibu Katibu Karibona amesisitiza  suala la nidhamu na ufanisi wa kazi kwa maafisa hao huku akiwasisitiza weledi wa kufanya kazi za Tume kwa kuzingatia Sheria na taratibu za  tume hiyo.

Halikadhalika, Naibu Karibona amehimiza ushirikiano wa pamoja ili kufanikisha kazi za Tume.