THBUB KUTOA ELIMU KWA WANANCHI WANAFUNZI NA WATENDAJI WA KATA ZA WILAYA KATIKA MKOA WA NJOMBE

Kamishna wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) Mhe. Dkt. Thomas Masanja, amefika katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Njombe na kukutana na Mkuu wa Mkoa huo, Mhe. Anthony Mtaka.
Katika ziara yake, Dkt. Masanja ameeleza kuwa THBUB imefika katika mkoa wa Njombe kwa lengo la kutoa elimu umma kuhusiana na maswala ya haki za binadamu na utawala bora, kusikiliza na kupokea malalamiko ya Wananchi yanayohusiana na uvunjifu wa haki za binadamu na ukiukwaji wa misingi ya utawala bora kupitia mikutano ya hadha, pia kuanzisha klabu za haki za binadamu mashuleni.
Aidha THBUB itatembelea maeneo wanapozuiliwa watu kama Vituo vya Polisi na Magereza kwa lengo la kuangalia uzingatiwaji wa viwango vya haki za binadamu katika maeneo hayo.
Akizungumza wakati wa mapokezi, Mhe. Mtaka amepongeza ujio wa Kamishna huyo na kueleza kuwa juhudi za THBUB ya Haki za Binadamu zinatoa mchango mkubwa katika kuongeza uelewa wa wananchi kuhusu haki zao. Amesema kuwa elimu hii ni muhimu kuwafikia makundi yote, hususan wanafunzi, kwani wao ndio wazazi na viongozi wa kesho.
"Tunapowafundisha haki za binadamu wakiwa mashuleni, tunajenga jamii inayoheshimu haki, utu na usawa kwa vizazi vijavyo," amesema Mhe. Mtaka