ADEM Logo
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA

Tunajenga utamaduni wa kuheshimu haki za binadamu, misingi ya utawala bora na utu wa mtu
ADEM Logo

THBUB KUFANYA UTAFITI WA KUWASAIDIA WANANCHI KUFIKIA HUDUMA ZA AFYA

01 Aug, 2024
THBUB KUFANYA UTAFITI WA KUWASAIDIA WANANCHI KUFIKIA HUDUMA ZA AFYA

 

Imeelezwa kuwa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB), katika mwezi Julai mpaka Septemba inategemea kufanya utafiti kuhusu nafasi ya mifuko ya skimu za afya katika kuwasaidia

wananchi kufikia huduma za afya ikiwa ni kutimiza majukumu yake katika kutoa huduma.

Hayo yameelezwa leo Julai 31,2024 Jijini Dodoma na Kamishna wa Tume hiyo Dkt.Tomas Masanja wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na utafiti katika huduma zinazotolewa na makampuni na mifuko ya Bima ya afya.

“Tunafanya tafiti hii kwa kuangalia moja ya haki za binadamu nchini ambayo ni haki ya afya, haki hii inaelezwa na mikataba ya kimataifa lakini inaelezwa vilevile na sheriazetu, bahati mbaya haipo moja kwa moja kwenye katiba lakini unapozungumzia haki ya kuhishj moja kwa moja utagusia haki ya afya” amesema.

Sambamba na hilo Dkt. Msanja amebainisha kuwa lengo la utafiti huo nikufanya tadhmini ya namna ambavyo skimu za bima ya afya zinazoongozwa na sheria ya Bima ya afya kwa wote zitasaidia wananchi kuweza kufikia huduma kuwepo kwa huduma na uwepo wa huduma bora.

“Tunajikita kwenye kusaidia kufikia huduma za afya kwasababu unapozungumzia haki ya afya maana yake unazungumzia jinsi ya kufikia huduma, uwepo wa huduma lakini uwepo huduma hizo pia unazungumzia ubora huduma zenyewe sasa sisi katika utafiti huu tumejikita tu katika eneo moja mbali ni jinsi gani sasa wananchiwataweza kuzifikia huduma hizi”amesema.

Amesema Tume inatambua  vyema jitihada za Serikali katika kuhakikisha uwepo wa huduma hizo ikiwemo ujenzi wa Zahanati na Hospitali katika kila mkoa hivyo uwepwa huduma hizo hivyo sio vitu vya kufanyia utafiti bali wanaangalia namna ambavyo wananchi wanaweza kuzifikia huduma hizo

kupitia skimu za bima ya afya.

“Lengo la sheria ya Bima ya afya kwa nikufanya wananchi wafikie hizi huduma na katika kufanya hiyo tadhmini tutajitahidi kuzitambua sheria zote ambazo zinajielekeza kuhusu skimu za bima yaafya, kanuni kama zipo na mipango kamaipo lakini tutafanya na uchambuzi wa kanuni hizo”Ameongeza

Pia katika utafiti huo amesema wataangalia namna ambavyo watu wanaelewa uwepo wa hizo skimu za bima ya afya pamoja na umuhimu wake pamoja na kutambua ni kwa kiwango gani walioko katika mifuko ya bima ya afya wanaridhika na huduma wanazopewaambapo 15% pekee ya watanzania ndiyowaliopo kwenye skimu za bima ya afya.

Dkt. Masanja ameongeza kuwa wanafanya hivyo kwa mamlaka na jukumu walilonalo na watahakikisha matokeo watakayoyapata katika utafiti huo wanayafikisha kwa wa husika na yanafanyiwa kazi.