MASWI AITAKA THBUB KUWA TAASISI YA MFANO
Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Eliakim Maswi amewataka watumishi wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) kufanya kazi kwa kuzingatia sheria za nchi, maadili na nidhamu ya kazi.
Maswi ametoa wito huo wakati akifungua Mkutano wa 23 wa Baraza la Wafanyakazi wa uliofanyika katika Ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma leo Februari 5, 2025 .
" kazi mliyonayo ni kuithibitishia Serikali kwamba mko tayari kutekeleza majukumu mliyopewa kwa mujibu wa sheria na mnatakiwa kuwa mfano bora wa kuigwa kwa kuwa taasisi inayolinda haki za binadamu na misingi ya utawala bora " amesisitiza Maswi
Awali akitoa neno la utangulizi, Mwenyekiti wa Baraza hilo, Bw. Patience Ntwina amesema kuwa lengo la mkutano huo ni kupitia na kujadili taarifa za utekelezaji wa shughuli za Tume kwa mwaka wa fedha 2023/2024 na 2024/2025 na na mapendekezo ya mpango na bajeti ya mwaka 2025/2026.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa baraza la wafanyakazi (TUGHE) tawi la Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Bw. Pontian Kitorobombo, kwa niaba ya Wajumbe wa baraza hilo amemshukuru Katibu Mkuu kwa kufungua Mkutano huo na kuahidi kuwa wajumbe watahakikisha wanaisaidia taasisi kuwa kwa kujadili masuala yenye kuleta tija kwa taasisi na watumishi