ADEM Logo
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA

Tunajenga utamaduni wa kuheshimu haki za binadamu, misingi ya utawala bora na utu wa mtu
ADEM Logo

WATENDAJI MBULU WATAKIWA KUFIKISHA ELIMU YA HAKI ZA BINADAMU KWA WANANCHI

24 Mar, 2025
WATENDAJI MBULU   WATAKIWA KUFIKISHA ELIMU YA HAKI ZA BINADAMU KWA WANANCHI

Makamu Mwenyekiti Wa Tume ya Haki za binadamu na Utawala bora Mhe. Mohamed Khamis  Hamad amewasisitiza Watendaji wa kata Halmashauri ya Wilaya ya Mji Mbulu kuendelea kuwaelimisha wananchi kuachana na mila na desturi potofu ili kuepuka uvunjifu wa Haki za binadamu.

"Watendaji mna wajibu wa kuhakikisha wananchi wanaelimishwa ili kulinda kizazi cha hapo baadae". Alisema Mhe. Mohamed 

Rai hiyo imetolewa  katika semina ya mafunzo ya Watendaji wa hao yaliyofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Mji wa Mbulu Machi 21, 2024

Sambamba na wito huo, Mhe. Mohamed amewataka Watendaji wa Kata kufuata Misingi na Utawala bora wakati wa utekelezaji wa majukumu yao  ikiwemo usawa katika utatuzi wa Migogoro.

Awali, akitoa mada ya haki za binadamu na utawala bora, Afisa Mhunguzi Mkuu Msaidizi, Bw.Halfan Botea amezitaja haki za binadamu kuwa ni pamoja na haki ya usawa,  kuishi, kupata elimu,  kuabudu,  faragha, kujumuika na kutoa maoni.

Mafunzo ya haki za binadamu na  utawala bora kwa Watendaji kata wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu  ni mwendelezo wa mafunzo yanayotolewa kwa watendaji kata mkoa wa Manyara