ADEM Logo
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA

Tunajenga utamaduni wa kuheshimu haki za binadamu, misingi ya utawala bora na utu wa mtu
ADEM Logo

Ziara ya UJumbe wa Ubalozi wa Norway THBUB

11 Oct, 2024
Ziara ya UJumbe wa Ubalozi wa Norway THBUB

Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) kushirikiana na ubalozi wa Norway nchini Tanzania.
Hayo amesema Bi.Ingrid Norstein wakati alipotembelea Makao Makuu ya Ofisi za THBUB zilizopo Mtaa wa Kilimani Jijini Dodoma Oktoba 10, 2024.

Bi. Norstein amesema kuwa, kwa zaidi ya miaka sitini (60)Tanzania na Norway zimekuwa na ushirikiano mzuri kwenye maeneo ya Biashara na Siasa, pia zimekuwa zikishirikiana katika miradi mbalimbali.


 Bi. Norstein aliongeza kwa kusema kuwa Norway pia iko tayari kushirikiana na THBUB katika masuala ya siasa hususani katika eneo la utawala (Governance).

Kwa upande wake Mwenyekiti wa THBUB Mhe. Mathew P. M.  Mwaimu (Jaji Mstaafu) ametaja  ambayo  THBUB inaweza kushirikana na Ubalozi   huo katika kulinda, kukuza na kuhifadhi haki za binadamu nchini, ikiwemo Kuwajengea uwezo Maafisa Uchunguzi  wa THBUB ,Utekelezaji na Uandaaji wa Mpango Kazi wa Kitaifa wa Biashara na  Haki za Binadamu  (NAP-BHR), utoaji elimu kwa umma, ufuatiliaji wa mapendekezo ya UPR (Universal Periodic Review), Hali ya Utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo endelevu hususan lengo namb.16, pamoja kuwezesha THBUB kupata vitendea kazi na Rasilimali fedha.


Aidha,Mhe.Mwaimu ameueleza  ujumbe huo kuwa THBUB inatarajia  kufanya uchunguzi katika Mikoa 16 ikiwa ni moja ya utekelezaji  wa majukumu yake katika kulinda na kusimamia haki za binadamu.
“Chunguzi  hizi tunazotegemea kuzifanya hivi karibuni ni chunguzi maalum zinazohusu matukio ya  kupotea kwa watu’’ amesema Mhe. Mwaimu.

 Kwa hatua nyingine Bi Norstein ametoa pongezi kwa THBUB kwa mapokezi mazuri  pamoja na ukarimu walionesha.

“Asanteni sana”amesema Bi.Norstein


Kikao hicho pia kilihudhuriwa na Kamishna wa THBUB  Mhe. Dkt.Thomas Masanja, Katibu Mtendaji wa THBUB Bw. Patience K. Ntwina na Afisa Uchunguzi Mkuu Bw. Fadhili Muganyizi na Bw. Victor Malunde kutoka ubalozi wa Norway nchini Tanzania.