WAKAZI WA DODOMA NA MIKOA JIRANI WAFIKA BANDA LA THBUB MAONESHO YA NANENANE
                                Wananchi wa Mkoa wa Dodoma na Mikoa Jirani wanaendelea kufika katika Banda la Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora kufahamu haki zao na wajibu katika kulinda na kukuza haki za binadamu nchi ni.
Akizungumza  na wananchi waliotembelea Banda la THBUB Afisa Uchunguzi Mkuu Msaidiizi  Bw. Halfan Botea amesema kuwa  haki za binadamu ni za kila mtu ,kila mahali kwasababu  ya kuwa ni binadamu.Zinavuka mipaka ya rangi, jinsia,taifa  na Imani,zinahakikisha usawa  na heshima ya asili kwa wote.
"Haki hizi binadamu huzaliwa nazo na kila mtu anatakiwa kuzipata"amesema Bw.Botea
Pia Bw.Botea  ameweleza wananchi  hao kuwa haki za binadamu  haziwezi kuondolewa au kubatilishwa,isipokuwa 
katika hali maalum za kisheria,kama vile kufungwa  kwa kufuata utaratibu unaostahili.
Aidha,Bw.Botea ameeleza wajibu wa kila mtu katika  kupata haki kupata.
“haki inaendana na wajibu ,kila mtu anahaki ila haki hizo lazima ziendane na wajibu’amesema Bw.Botea
Kwa upande wake Rahimu Juma Mkazi wa Dodoma ametoa shukrani kwa THBUB kutoa elimu hiyo
"Elimu niliyopata leo ni msaada kwa wengine kujua haki zao"amesema Bw.Juma
Maadhimisho  ya Maonesho  Nanenane Kitaifa yamefunguliwa Agosti  2 ,2025 na Makamu wa Rais Dkt.Isdory Philip Mpango  katika Viwanja vya Nzuguni Jijini Dodoma.

