ADEM Logo
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA

Tunajenga utamaduni wa kuheshimu haki za binadamu, misingi ya utawala bora na utu wa mtu
ADEM Logo

THBUB yatoa Rai kwa Umma Kutowaficha Watu wenyeulemavu

03 Dec, 2024
THBUB yatoa Rai kwa Umma Kutowaficha Watu wenyeulemavu

Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB), imetoa rai kwa umma,kutowaficha watu wenye ulemavu kwakuwa pamoja na hali yao bado ni binadamuna wanastahili kutambuliwa bila ya kujalihali yao ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa kwa mamlaka za Serikali zilizopo kwenye maeneo wanayoishi juu ya vitendo vya ukatili, ubaguzi, udhalilishaji, unyanyasaji, unyanyapaaji kwa watu wenye ulemavu.

Rai hiyo imetolewa leo Disemba 3,2024 Jijini Dodoma na Mwnyekiti wa tume hiyo Jaji Mstaafu Mathew Mwaimu wakati akitoa tamko kuhusu Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Watu wenye Ulemavu ambapo kitaifa mwaka huu yamefanyika kitaifa Jijini la Dar es Salaam na kuongozwa na kauli mbiu isemayo “Kukuza uongozi wa watu wenye ulemavu kwa ajili ya Mustakabali jumuishi na endelevu”.

“Kauli mbiu hii inaikumbusha Serikali kuona umuhimu wa kuongeza jitihada za dhati kwa kutoa fursa za uongozi kwa watuwenye ulemavu ili waweze kushiriki na kuongoza kikamilifu shughuli mbalimbali

zikiwemo za Kisiasa, Kiuchumi na Kijamii” amesema Mhe.Mwaimu.

Aidha, ameongeza kuwa THBUB inatambua jitihada mbalimbali zilizofanywa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar katika kulinda na kutetea haki za Watuwenye Ulemavu nchini ikiwa ni pamoja na kuwateua watu wenye ulemavu kushika nafasi mbalimbali za uongozi, kuweka mazingira rafiki kwa watu wenye ulemavukwa kufanya maboresho katika ujenzi wa majengo mapya ya umma ambayo yanajengwa kwa kuzingatia ufikikaji kwa makundi ya Watu wenye Ulemavu.

Mbali na hayo ameendeleea kutoa rai kwa umma, kutowaficha watu wenye ulemavu

kwa kuwa pamoja na hali yao bado ni binadamu na wanastahili kutambuliwa bilaya kujali hali yao ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa kwa mamlaka za Serikali zilizopo kwenye maeneo wanayoishi juu ya vitendo vya ukatili, ubaguzi, udhalilishaji, unyanyasaji, unyanyapaaji kwa watu hao.

 

“Pia, wito unatolewa kwa wananchikuachana na imani, mila, desturi na mitazamo potofu ambayo huwafanya watuwenye ulemavu kujiona hawakubaliki,hawawezi na hawana mchango kwa jamii inayowazunguka na Taifa kwa ujumlakatika shughuli zinazohusu

Maendeleo”amesema Mhe.Mwaimu

Siku ya kimataifa ya watu wenye ulemavu ni matokeo ya Azimio la Baraza Kuu laUmoja wa Mataifa Na. 47/3, 1992 ambapo ilipitishwa kuwa Disemba 3 ya kila mwakani Siku ya Maadhimisho ya Watu wenye Ulemavu Duniani yakiwa yanalenga kuhamasisha jamii kutambua haki na fursasawa na ushiriki wa watu wenye ulemavu katika masuala ya maendeleo, mahitaji yao,changamoto zinazowakabili na kutafutanamna ya kukabiliana nazo.