THBUB YASHIRIKI MAADHIMISHO YA SIKU YA WAFANYAKAZI DUNIANI MEI MOSI, 2025.

Watumishi wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) Tawi la Dar es salaam wameshiriki katika Maadhimisho ya siku ya wafanyakazi Duniani ( Mei mosi) ambayo kimkoa yamefanyika katika Wilaya ya Kinondoni kwenye Viwanja vya Tanganyika Packers Kawe, Jijini Dar es salaam.
Katika Maadhimisho hayo Mgeni Rasmi Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Bw. Albert Chalamila amewataka Wafanyakazi kutambua wajibu wao na kwamba wao ndio taswira ya Serikali.
“Wafanyakazi tunaposherehekea siku hii tutambue kuwa sisi ndio tumebeba taswira ya Serikali kwani mfanyakazi mmoja anaweza kusababisha Serikali ichukiwe au ipendwe, hivyo wafanyakazi wote tuendee kufanya kazi kwa uaminifu na imani kwani Serikali inatujali na kutupenda” amesema Bw. Chalamila
Aidha, Bw. Chalamila amewataka wafanyakazi wote kutekeleza kauli mbiu ya siku ya leo kwa kushiriki kikamilifu katika Uchaguzi Mkuu ujao kwa kujiandikisha na kuchagua Madiwani, Wabunge pamoja na Rais.
Maadhimisho ya Mei Mosi 2025 yalikuwa na kauli mbiu isemayo “Uchaguzi Mkuu 2025, utuletee Viongozi wanaojali Haki na Maslahi ya Wafanyakazi, sote tushirik