ADEM Logo
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA

Tunajenga utamaduni wa kuheshimu haki za binadamu, misingi ya utawala bora na utu wa mtu
ADEM Logo

THBUB YAPOKEA MREJESHO WA UKUSANYAJI MAONI

15 Aug, 2024
THBUB YAPOKEA MREJESHO WA UKUSANYAJI MAONI

Leo 12 Agosti, 2024 Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora imepokea mrejesho wa kazi zilizifanywa na kila kundi katika maeneo ya vipaumbele ya Uandaajiwa Mpango Kazi wa Kitaifa wa Haki za Binadamu na Biashara.

Lengo la kikao hicho ni kubainisha maeneo yanayohitaji muitikio wa haraka waTHBUB ambayo hayahusiki moja kwa moja na Mpango kazi wa Kitaifa wa Haki zaBinadamu na Biashara.

 Aidha kila kundi lilipata nafasi ya kuwasilisha taarifa sambamba na kubainisha maeneo yanayohitaji kufanyiwa kazi haraka.

Kikao hicho kiliongozwa na Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Mhe. Mathew Mwaimu (Jaji Mstaafu) washiriki wengine ni Makamu Mwenyekiti

wa THBUB ,Mhe. Mohamed Khamis Hamad, Kaminshna Mhe.Dkt.Thomas Masanja, Mhe.Amina Talib Ali,Menejimenti na Washiriki kutoka kila kundi.

Aidha washiriki wa makundi walioko Dar es Salaam akiwemo Kamishna Mhe. Nyanda Shuli na watumishi wengine wameshiriki kikao hicho kupitia Zoom Meeting.