ADEM Logo
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA

Tunajenga utamaduni wa kuheshimu haki za binadamu, misingi ya utawala bora na utu wa mtu
ADEM Logo

THBUB YALAANI WIMBI LA MAUJAI YA KIKATILI

02 Sep, 2024
THBUB YALAANI WIMBI LA MAUJAI YA KIKATILI

Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB), imesema kuwa mauaji ambayo yameendelea kushika kasi licha ya jeshi la polisi kufanya jitihada za kuwakamata watahumiwa na kuwafikisha katika vyombo vya sheria imeweza kubaini visababishi mbalimbali ikiwemo ulipaji kisasi na imani za kishirikina.

Hayo yamebainishwa Agosti 30,2024 Jijini Dodoma na Mwenyekiti wa Tume Mhe. Mathew Mwaimu (Jaji Mstaafu) wakati akizungumza na Waandishi wa habari kuhusu kulaani wimbi la mauaji nchini.

“Mamlaka za Serikali za Mitaa katika ngazi zote ziwe na mipango madhubuti ya kuhakikisha kunakuwepo na taratibu za kuimarisha ulinzi wa usalama wa raia, kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi katika maeneo yao ikiwa ni pamoja na kuchukua hatua za mapema katika kushughulikia matukio ya uhalifu kwa kushirikiana na Mamlaka husika”amesema Mhe.Mwaimu

Mhe. Mwaimu amesisitiza pia wananchi wajenge utamaduni wa kuheshimu sheria za nchi na haki za binadamu, watambue namna bora ya kupata suluhu ya migogoro inayowakabili katika ngazi zote za jamii, na kushughulikia migogoro hiyo kwa mujibu wa sheria na taratibu zilizowekwa badala ya kujichukulia sheria mikononi.

Mhe.Mwaimu ametoa wito kwa, Asasi za Kiraia na vyombo vya habari kuendelea kutoa elimu kwa umma kuhusu taratibu zilizopo za namna ya kushughulikia masuala mbalimbali ya kijamii kupitia sheria, na hivyo kulinda haki za binadamu na utu wa mtu.

Aidha, Mhe.Mwaimu amesema pia matukio hayo ya mauaji yamekuwa yakiripotiwa na vyanzo mbalimbali vya taarifa hususani vyombo vya habari na taarifa kutoka jeshi la polisi nchini.

“Mara kadhaa Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan amekua akilaani na kukemea vitendo hivyo vya mauaji na sisi kama Tume ya haki za Binadamu na Utawala Bora na wadau wengine wameshiriki katika mijadala kupitia vyombo vya habari”amesema Jaji Mwaimu

Mwisho, THBUB inatoa pole kwa ndugu, jamaa na wanafamilia waliopoteza wapendwa wao katika matukio haya na kwa waliopatikana na majeruhi Mwenyezi Mungu aendelee kuwapa faraja.