THBUB YAENDELEA KUTOA ELIMU YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA KWA WATENDAJI KATA
29 Jan, 2025
![THBUB YAENDELEA KUTOA ELIMU YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA KWA WATENDAJI KATA](http://chragg.go.tz/uploads/news/883c90c3e56b03e9483827809c0851b1.jpeg)
Ujumbe wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala (THBUB) ukiongozwa na Makamu Mwenyekiti Mhe. Mohamed Khamis Hamad,umetoa mafunzo kwa Watendaji wa Kata kutoka Kata zilizopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi, leo Januari 27, 2025 katika Ukumbi wa Mikutano uliopo katika Ofisi za Halmashauri hiyo.
Aidha, Mafunzo hayo yamelenga kuwakumbusha Watendaji hao namna ya kuheshimu haki za binadamu na kuzingatia misingi ya utawala bora wakati utekelezaji wa majakumu yao ikiwemo kuwashirikisha wananchi katika masuala mbalimbali yanayowahusu
Pia, Watendaji hao wamepata nafasi ya kuuliza maswali sambamba na kuelezea changamoto wanazokutana nazo wakati wa kutekeleza majukumu yao ya kila siku