ADEM Logo
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA

Tunajenga utamaduni wa kuheshimu haki za binadamu, misingi ya utawala bora na utu wa mtu
ADEM Logo

THBUB yaendelea kuchakata maoni ya mpango kazi wa haki za binadamu na biashara

16 Oct, 2024
THBUB yaendelea kuchakata maoni ya mpango kazi wa haki za binadamu na biashara

ume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB)  imeendelea na Mchakato wa Uandaaji wa Mpango Kazi wa Kitaifa wa Haki  za Binadamu  na Biashara wenye lengo la kuweka  mazingira bora kwa  Wafanyabiashara kuzingaita haki za binadamu wakati wakifanya biashara zao.

Hayo amesema Makamu Mwenyekiti wa THBUB Mhe. Mohamed Khamis Hamad wakati wa kifungua  Kikao Kazi cha kupitia maoni yaliyokusanywa kutoka kwa wadau mbalimbali, kikao hicho kilifanyika Oktoba 15, 2024 Jijini Arusha.

Mhe. Mohamed amesema kuwa THBUB kwa  kushirikiana na wadau wengine imefanikiwa kukusanya maoni ya wadau  kupitia vikao na mikutano ya hadhara na wananchi wanaoishi maeneo ya uwekezaji ili kupata uhalisia.

“Tumefanikiwa kupita maeneo ya Viwanda, Shughuli za uvuvi, Mahotelini na hata maeneo ya Uchimbaji wa Madini na  kuzungumza na wafanyakazi na wananchi wanaozunguka maeneo hayo ”amesema Mhe. Mohamed

Aidha, Mhe. Mohamed ameongeza kwa kusema kuwa miongoni mwa changamoto zilizojitokeza  katika ukusanyaji wa maoni hayo ni wafanyakazi wengi kutokua na Mikataba ya Kazi, pamoja na uwepo wa migogoro baina ya wawekezaji na jamii inayowazunguka.

“Uandaaji wa Mpango Kazi huu utasaidia kuboresha maeneo  ambayo  tumeona yamekua na changamoto”amesema Mhe. Mohamed

Naye ,Mkurugenzi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) Dkt. Anna Henga amesema kuwa kwa miaka kadhaa kituo hicho kimekuwa kikifanya kazi ya Utetezi wa haki za binadamu katika sekta ya biashara na uchechemuzi wa Sera na Sheria kuhakikisha Mikataba na Miongozo ya Kimataifa pamoja na Sheria za nchi zinazohusiana na biashara zinatekelezwa kwa kufuata misingi ya haki za binadamu.

“Katika mchakato huu wa kutengeneza Mpango Kazi wa Biashara na Haki za Binadamu, LHRC imeshiriki  kikamilifu kama sehemu ya timu ya wataalamu wa Uandaaji  wa Mpango kazi huo” amesema Dkt. Anna

Kwa upande wake Bi. Joyce Deloge, Mwakilishi kutoka Shirika  la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP)  ameipongeza Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa  Tanzania kwa kuchukua hatua ya kuandaa Mpango kazi wa haki za Binadamu na Biashara ambao utakua  ni msaada mkubwa wa kusimamia masuala ya haki za binadamu katika biashara.

Pia Bi. Joyce ameeleza  zaidi kuwa nchi nyingi siku hizi zimekuwa wazi ambapo upelekea wafanyabiashara kuingia nakufanya shughuli zao bila kuzingatia taratibu za nchi husika.

“Mpango kazi huu  utasaidia kulinda na kukuza haki za binadamu katika sekta ya biashara nchini Tanzania “amesema Bi.Joyce

Awali Katibu Mtenda wa THBUB Bw. Patience Ntwina amesema kuwa THBUB na wadau wengine walipitia nyaraka mbalimbali ambazo ni Sera, Sheria, Mipngo na Mikakati iliyopo nchini kuhusiana na biashara na uwekezaji, kukusanya maoni kutoka kwa wadau mbalimbali maoni ya wadau kwa upande wa Tanzania Bara na Zanzibar na kuangalia uzoefu kutoka nchi nyingine ili kueza kufahamu changamoto wanazokutana nazo katika eneo hili.

Bw. Ntwina amesema kuwa kupitia Kikao Kazi hicho cha Siku Nne (4) wataalamu watatatoka na Rasimu ya Awali ya Mpango Kazi wa Kitaifa wa Biashara na Haki za Binadamu ambao utakuwa na maeneo ya vipaumbele na majukumu ya kila mdau muhimu  katika uboreshaji wa haki za binadamu katika sekta ya biashara nchini.