THBUB YAELEZA NAFASI YAKE KATIKA UCHAGUZI MKUU

Kamishna wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) Mhe. Khatib Mwinyichande, amesema kuwa THBUB ina jukumu la kufanya ufuatiliaji wa Uchaguzi Mkuu kwa lengo la kuangalia uzingatiwaji wa haki za binadamu na misingi ya utawala bora ili kuhakikisha kunakuwa na uchaguzi huru na haki.
Akizungumza na waandishi wa habari katika Maonesho ya 49 ya kimataifa ya Biashara "Sabasaba" kwenye banda la THBUB. Mhe. Mwinyichande alibainisha kuwa THBUB ina jukumu la kukuza na kulinda haki za binadamu na utawala bora nchini, jambo linaloifanya kuwa na nafasi ya moja kwa moja katika kufuatilia mchakato wa uchaguzi.
"Uchaguzi si tukio la kisiasa pekee, bali ni jambo linalogusa maisha ya watu pamoja na haki za msingi za wananchi, kwa kuwa nchi yetu ni ya kidemokrasia, viongozi wake hupatikana kwa kuteuliwa au kuchaguliwa kupitia uchaguzi, hivyo jukumu la THBUB ni kuhakikisha kwamba kunakuwepo na uchaguzi huru na wa haki kwa kuhakikisha Sheria zinafuatwa na haki za binadamu zinalindwa katika kila hatua ya uchaguzi," amesema.
Mhe. Mwinyichande aliongeza kuwa THBUB ni miongoni mwa taasisi zinazoangalia uchaguzi kuanzia hatua kujiandikisha katika daftari la kudumu la mpiga kura hadi siku ya kutangazwa matokeo ya uchaguzi na baada ya matokeo, huku akisisitiza kuwa THBUB itakuwa ikifuatilia mwenendo wa uchaguzi na kuandika taarifa itakayowasilishwa kwa mamlaka husika.
"Katika kila hatua ya uchaguzi, THBUB inafuatilia, changamoto zitakazobainika zitawasilishwa katika mamlaka husika kwa ajili ya kutatuliwa. Hii ni njia mojawapo ya kulinda haki za wananchi," aliongeza.
Kuhusu Maonesho ya Sabasaba
Akizungumzia ushiriki wa THBUB kwenye Maonesho ya Sabasaba, Mhe. Mwinyichande alisema ni sehemu ya kutekeleza jukumu lake la kuhamasisha hifadhi na ulinzi wa haki za binadamu katika jamii kwa kutoa elimu kuhusu haki za binadamu na utawala bora,
"Maonesho haya yanaisadia THBUB kukutana moja kwa moja na wananchi, kupokea malalamiko yao, kutoa elimu ya haki za binadamu, na kuwaeleza kuwa sisi ni watetezi wao pale wanapokwazwa na kukosa haki zao," amesema mhe.
Amesisitiza kuwa elimu hiyo inawasaidia wananchi kufahamu kuwa haki zao na namna ya kuzidai kwa kuzingatia Sheria na taratibu zilizowekwa, na kwamba THBUB ipo kwa ajili ya kuhakikisha kuwa hakuna mwananchi anayebaguliwa au kunyimwa haki zake kwa misingi yoyote.
Maonesho ya Sabasaba yamekuwa yakitumika na taasisi mbalimbali kama jukwaa la kuwasiliana moja kwa moja na wananchi. THBUB inatumia fursa hiyo kuongeza uelewa kwa umma kuhusu haki za msingi, utawala bora na njia sahihi za kudai ha