ADEM Logo
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA

Tunajenga utamaduni wa kuheshimu haki za binadamu, misingi ya utawala bora na utu wa mtu
ADEM Logo

Tanzania kunufaika na Mradi wa”Sustainable Ocean Phase II"

09 Jul, 2024
Tanzania kunufaika na Mradi wa”Sustainable  Ocean  Phase II"

Tanzania  ni miongoni mwa nchi zitakazo nufaika na mradi wa “Sustainable Ocean  Phase II"unaosimamiwa na Taasisi ya Kitaifa ya Haki za Binadamu nchini Denmark(Danish Institute of Human Rights).

Hayo yamebainishwa na  Mshauri Mkuu wa Taasisi hiyo Bi.Carol Rask wakati walipotembelea Ofisi ya Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora hivi karibuni Jijini Dodoma.

 Bi.Carol alisema mradi huo unaotarajiwa   kutaekelezwa kwa muda wa miaka minne unafadhiliwa na SIDA.

“mradi huo umelenga kuimarisha ulinzi wa mazingira kwa wavuvi wadogo na jamii zinazowazunguka”alisema Bi.Carol

Aidha Bi Carol alisema katika kutekeleza mradi huo wamefanya ziara nchini Tanzania iliyolenga  kutafuta wadau mbalimbali ambapo moja ya wadau hao ni Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora.

Bi Carol alisema wametembelea Tanzania ili kujifunza zaidi kuhusu maeneo yanayoweza kuzingatiwa ili kutekeleza mradi huo ikiwemo kukutana na Wadau mbalimbali ili kupata maoni yao  pamoja na kuhakikisha watendaji wa Serikali na Sekta binafsi wanachukua hatua za kuimarisha haki za binadamu  kwa wavuvi wadogo na jamii inayowazunguka kwa kuzingatia  sheria za kitaifa,Sera na mipango inayohusiana na utawala wa wavuvi.

Naye,Mratibu Miradi  Tume ya Haki za Binadamu  na Utawala Bora  Bi.Jovina Muchunguzi  alisema  kuwa Tume inaendelea na mchakato wa uwandaaji wa Mpango Kazi wa Kitaifa wa Haki za Binadamu na Biashara  kwa kushirikiana  na wadau kutoka Serikalini na Sekta binafsi .

"Tume imeshakutana na wadau hao na kuwaeleza hatua mbalimbali zilizofanyika  za uandaaji wa mpango kazi huo"alisema Bi.Jovina

Aidha ,Bi Jovina alisema kuwa  Tume,katika mchakato  wa uandaaji wa Mpango kazi wa Kitaifa wa Haki za Binadamu  na Biashara  eneo moja la kipaumbele ni kilimo na uchumi wa bluu ndani yake kuna shughuli  za uvuvi.

"Eneo hili ni muhimu  katika maisha ya watanzania na katika mpango unaondaliwa"alisema Bi.Jovina

Kwa hatua nyingine  ujumbe huo ulieleza kuwa ipo tayari  kushirikiana  na Tume katika masuala ya Mafunzo,Tafiti,Kuandaa miongozo ya kusimamia  haki za binadamu  na masuala mengine.Ugeni huo  ulipokelewa na Makamu Mwenyekiti  wa Tume ya Haki za Binadamu  na Utawala Bora Mhe.Mohamed  Khamis  Hamad,Katibu Mtendaji Bwa.Patience  Ntwina na baadaye mazungumzo hayo  kuongozwa na Bi. Jovina Muchunguzi pamoja na Bw.Constatine Mugusi.