ADEM Logo
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA

Tunajenga utamaduni wa kuheshimu haki za binadamu, misingi ya utawala bora na utu wa mtu
ADEM Logo

Afisa wa Tume atoa Elimu kuhusu Utawala Bora(Dhana, Misingi na Umuhimu) Chuoni.

13 Feb, 2023
Afisa wa Tume atoa Elimu  kuhusu Utawala Bora(Dhana, Misingi na Umuhimu) Chuoni.

Bw. Said Zuberi, Afisa Uchunguzi Mwandamizi kutoka Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) akitoa elimu kuhusu Utawala Bora (Dhana, Misingi na Umuhimu) kwa wanachama wa Jumuiya ya Haki za Binadamu kutoka Chuo Kikuu cha Dodoma iliyofanyika katika Ukumbi wa LM 8 Ndaki ya Elimu tarehe 4 Februari, 2023. Watoa Mada wengine walikuwa Bi. Euphrasia Peragius, Afisa Sheria kutoka Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu ambaye alitoa Mada kuhusu Haki za Binadamu na Wakili wa kujitegemea Bw. Michael Mushi yeye alitoa Mada kuhusu Haki za Binadamu na Mtandao. Tukio hilo liliambatana na  uzinduzi wa kipeperushi cha Jumuiya hiyo kinachoelezea Kuhusu Jumuiya: Malengo, Mikakati, Majukumu na Utaratibu wa Kujiunga.