ADEM Logo
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA

Tunajenga utamaduni wa kuheshimu haki za binadamu, misingi ya utawala bora na utu wa mtu
ADEM Logo

Ziara ya Rais wa Mahakama ya Afrika Haki za Binadamu THBUB

08 Dec, 2024
Ziara ya Rais wa Mahakama ya Afrika Haki za Binadamu THBUB

Rais wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu (AfCHPR) Mhe. Imani Daud Aboud ametembelea Makao makuu ya ofisi ya Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora iliyopo Mtaa wa Kilimani Jijini Dodoma Desemba 04,2024.

Akizungumza wakati wa ziara hiyo Mhe.Aboud amesema kuwa  lengo la ziara ofisini hapo ni kufanya mazungumzo na Uongozi wa THBUB sambasamba na kuifahamisha majukumu ya Mahakama hiyo.

Mhe Aboud amesema kuwa Mahakama hiyo inajukumu kubwala la kukuza na kulinda haki za binadamu

“Mahakama hii inafanya kazi kama mahakama nyingi,ila ili uweze shauri liweze kusikilizwa,lazima mteja apitie hatua zote”amesema Mhe.Aboud

Aidha, Mhe. Aboud amegusia  pia suala la Tanzania kujiondoa katika tamko linaloruhusu Mahakama kupokea Mashauri yanayopelekwa na Wananchi au mashirika yasiyo ya kiserikali,Kutokana THBUB ni mdau muhimu katika kuhakikisha dhumuni la kuanzishwa kwa Mahakama linatimizwa.

“Tumezungumza na THBUB ili iweze kujihusisha na huu mchakato wa kuona kwamba Tanzania inaweka mkazo suala la kurudisha hilo tamko ili kuwaruhusu watanzania waweze kupata huduma za mahakama yao kwani Mahakama ya Afrika ni Mahakama ya waafrika wote na Nchi zote za Umoja wa Afrika zinachangia fedha kwa ajili ya uendeshaji wa shughuli za Mahakama hiyo” amesema Mhe. Aboud.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa THBUB Mhe. Mathew Mwaimu (Jaji Mstaafu) amesema kuwa zipo changamoto zilizosababisha Tanzania kujitoa katika tamko hilo na THBUB inaona kuwa changamoto hizo zinaweza kutatuliwa na Tanzania ikaweza kurudisha tamko hilo ili wananchi waweze kunufaika na Mahakama hiyo.

 

 Aidha Mhe. Mwaimu amesema kuwa kutokana na jitihada zinazofanywa na Mahakama hiyo ikiwa na pamoja na kufanya ziara kwa viongozi wakuu wa Nchi, THBUB inaamini kuwa jitihada zitaweza kufanikiwa na muda si mrefu Serikali itaweza  kurudisha tamko hilo ili watanzania waendelee kufurahia huduma hizo.

ma hii na Serikali ya Tanzania zinaweza kukaa kwa pamoja na kutatua changamoto zilizopo na kuweza kurudisha tamko hilo la kuruhusu wananchi Kwenda katika mahakama hiyo” amesema Mwenyekiti wa THBUB.

Katika ziara hiyo Rais Aboud aliambatana na Makamu wa Rais wa Mahakama hiyo Mhe.Modibo Sacko na Mhe. Jaji Duncan Gaswaga pamoja na watendaji wengine wa Mahakama.

Tanzania iliandika kusudio la kujiondoa katika tamko hilo Novemba 2020 katika ibara ya 34 (6) ya Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu ambayo inaruhusu  watu binafsi na asasi zisizo za kiserikali kuwasilisha mashauri ya Haki za Binadamu.