ADEM Logo
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA

Tunajenga utamaduni wa kuheshimu haki za binadamu, misingi ya utawala bora na utu wa mtu
ADEM Logo

THBUB NA DIHR WAENDELEA KUIMARISHA USHIRIKIANO WA KULINDA HAKI ZA WAVUVI WADOGO.

12 Jul, 2026
THBUB NA DIHR WAENDELEA KUIMARISHA USHIRIKIANO WA KULINDA HAKI ZA WAVUVI WADOGO.

Mshauri kutoka Taasisi ya Kitaifa ya Haki za Binadamu ya Denmark (Danish Institute for Human Rights – DIHR), Bi. Sofie Hansen, amekutana na Katibu Mtendaji wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB), Bw. Patience Ntwina, katika ofisi za Makao Makuu ya Tume Jijini Dodoma kwa mazungumzo yaliyolenga kuimarisha ushirikiano katika utekelezaji wa miradi ya haki za binadamu.

Ziara ya Bi. Hansen nchini Tanzania ni sehemu ya ushirikiano unaoendelea kati ya THBUB na DIHR katika utekelezaji wa Mradi wa Bahari Endelevu unaolenga kukuza mtazamo wa haki za binadamu katika usimamizi wa rasilimali za baharini, hususan kulinda na kuendeleza haki za wavuvi wadogo.

Kupitia mradi huo, THBUB imeimarisha uwezo wa ndani katika masuala ya haki za wavuvi wadogo, ikiwemo kufanya utafiti wa awali kuhusu haki zao katika ufikiaji, upatikanaji na usimamizi wa rasilimali za baharini.

Utafiti huo umebaini kuwepo kwa changamoto mbalimbali zikiwemo usimamizi shirikishi usioridhisha wa rasilimali za bahari, changamoto za haki za umiliki wa rasilimali, uchafuzi wa mazingira, athari za mabadiliko ya tabianchi, unyanyasaji wa kijinsia, mifumo isiyo imara ya utatuzi wa migogoro pamoja na kutokuwepo kwa mpango madhubuti wa matumizi ya bahari.

Aidha, utafiti umeonesha kuwa ongezeko la uwekezaji katika shughuli za uchumi wa buluu, utalii, nishati na uvuvi wa viwanda limeongeza ushindani wa matumizi ya maeneo ya pwani na bahari, hali inayowaathiri wavuvi wadogo katika kuendesha shughuli zao za kiuchumi na kujipatia kipato.

Katika ziara hiyo, Bi. Hansen pia anatarajiwa kushiriki kikao cha wadau wa sekta ya uvuvi kitakachofanyika Julai 9, 2026, Jijini Dodoma, kikihusisha wadau kutoka Serikalini, Asasi za Kiraia (AZAKI) na mashirika ya kimataifa kwa lengo la kujadili masuala mbalimbali yanayohusu haki za wavuvi wadogo na usimamizi endelevu wa rasilimali za baharini.

Akizungumza wakati wa mazungumzo hayo, Katibu Mtendaji wa THBUB, Bw. Patience Ntwina, ameishukuru DIHR kwa kuendelea kutoa ushirikiano na ufadhili wa kifedha katika utekelezaji wa Mradi wa Bahari Endelevu, hususan katika kuimarisha ulinzi na utetezi wa haki za wavuvi wadogo.

Bw. Ntwina amesisitiza kuwa THBUB itaendelea kuhimiza matumizi ya mtazamo wa haki za binadamu katika kuhakikisha upatikanaji, ufikiaji na usimamizi endelevu wa rasilimali za baharini, huku ikiendelea kuimarisha ushirikiano wake na DIHR katika kutekeleza majukumu hayo kwa manufaa ya wananchi.

slot gacor