ADEM Logo
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA

Tunajenga utamaduni wa kuheshimu haki za binadamu, misingi ya utawala bora na utu wa mtu
ADEM Logo

MAADHIMISHO YA MIAKA 63 YA UHURU TANZANIA BARA THBUB YA PANDA MITI

16 Dec, 2024
MAADHIMISHO YA MIAKA 63 YA UHURU TANZANIA BARA THBUB YA PANDA MITI

Watumishi Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) wameadhimisha Miaka 63 ya Uhuru kwa kupanda miti.

Akizungumza Kamishna wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Mhe. Amina Talib Ali mara baada ya zoezi la upandaji miti  lililofanyika katika Bustani ya THBUB iliyopo Nkuhungu, Dodoma.

Mhe. Amina amewahimiza watumishi wa Umma kupenda kujitolea kufanya kazi za Kijamii ikiwa ni pamoja na kulinda mazingira. 

“Niwapongeze Watumishi wote mlioweza kushiriki katika zoezi hili na niwaombe muendelee kujitoa katika shughuli za kijamii kama hizi kwani kazi hizi zinasaidia kulinda na kutunza mazingira yetu na kujenga mshikamano ambao ni matunda ya Uhuru" amesema Mhe. Amina.

Naye, Katibu Mtendaji wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Bw.Patience Ntwina amesema kuwa Mazingira yanamchango mkubwa sana katika kukuza Haki za Binadamu hivyo kupanda miti kutasaidia binadamu kuwa salama na kufurahia mazingira yanayomzunguka.

Ikumbukwe kuwa, Kila ifikapo tarehe 09 Disemba, Taifa linakumbuka na kuadhimisha Siku hii muhimu katika historia ya Tanzania Bara kwa namna ya kipekee kwani ndiyo siku ambayo Tanzania Bara ilipata Uhuru wake kutoka Serikali ya Mkoloni ya Uingereza. Hivyo kumekuwepo utamaduni wa kuiadhimisha siku hii Kwa kufanya matukio mbalimbali yanayotuleta pamoja.

 Maadhimisho ya Miaka 63 ya uhuru mwaka 2024, yalibebwa na kauli mbiu isemayo "Uongozi Madhubuti na Ushirikishwaji wa Wananchi ni Msingi wa Maendeleo yetu