ADEM Logo
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA

Tunajenga utamaduni wa kuheshimu haki za binadamu, misingi ya utawala bora na utu wa mtu
ADEM Logo

Kuelekea  Maadhimisho  ya  Siku ya Maadili na Haki za Binadamu Desemba  10,2024

08 Dec, 2024
Kuelekea  Maadhimisho  ya  Siku ya Maadili na Haki za Binadamu Desemba  10,2024

Kuelekea  Maadhimisho  ya  Siku ya Maadili na Haki za Binadamu Desemba  10,2024.

Ujumbe wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) umetembelea Gereza Kongwa lilipo katika  Halmashauri ya Wilaya Kongwa, Mkoani Dodoma, Desemba 6, 2024.

Akizungumza wakati wa ziara hiyo Kamishna wa THBUB Mhe. Amina Talib Ali amesema kuwa THBUB inajukumu la kukuza, kulinda na kuhifadhi haki za binadamu  na misingi ya utawala nchini, katika kutekeleza  majukumu hayo, THBUB inajukumu la kutembelea magereza na maeneo mengine wanapozuiliwa watu kwa lengo la kutathmini haki za watu wanaoshikiliwa katika maeneo hayo na kutoa mapendekezo kwa ajili ya kurekebisha matatizo yaliyopo.

"THBUB ina wajibu wa kuhakikisha haki za binadamu zinalindwa na kuhifadhiwa hata kwa watu  waliopo Vizuizini" amesema Mhe. Amina.

Naye,Kamshna wa Sheria na usimamizi wa Magereza CP. Nicodemus Tenga amesema kuwa uwepo wa ushirikiano mzuri wa Taasisi za Haki Jinai umesaidia kwa kiasi kikubwa kurahisisha shughuli za Magereza.

"Mifumo inasomana vizuri ambapo imepelekea kupunguza idadi ya Mahabusu katika gereza hilo"amesema CP Tenga.

Aidha, CP Tenga ameongeza kuwa Serikali imetenga fedha kwa ajili ya kujenga vyumba vya Mahakama Mtandao ambayo pia itasaidia katika uendeshaji wa mashauri kwa haraka sambamba na usimikaji wa mfumo wa utakaosaidia utunzaji wa taarifa.

Awali, Mkuu wa Gereza la Kongwa SSP. Tekla Erasto amesema kuwa Gereza hilo linajishughulisha na Kilimo, Ujenzi, Ufugaji na Ufuatuaji Matofali na elimu ya watu wazima.

Pia SSP.Erasto ameushukuru ujumbe huo kwakupeleka mahitaji muhimu kwa Wafungwa na Mahabusu.

“Mahitaji haya yatatumika kwa walengwa kama ilivokusudiwa,nashukuru”amesema ssp.Erasto

ujumbe wa THBUB uliambatana na Wawakilishi kutoka Wizara ya Mambi ya Ndani, Wizara ya Katiba na Sheria, Ofisi ya Taifa ya Mashtaka ,Jeshi la Polisi,Tume ya Utumishi wa Umma, Mahakama na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU).

Kwa hatua nyingine ujumbe huo ulikabidhi  Mahitaji mbalimbali kwa Wafungwa na Mahabusu ikiwemo Sabuni, Dawa za Mswaki, Blanketi na Taulo za Kike.