ADEM Logo
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA

Tunajenga utamaduni wa kuheshimu haki za binadamu, misingi ya utawala bora na utu wa mtu
ADEM Logo

Ushiriki wa THBUB katika Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani 2023

05 May, 2023
Ushiriki wa THBUB katika Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani 2023

Baadhi ya Watumishi wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Ofisi Kuu ya Dodoma wakipita katika mitaa mbalimbali ya jijini Dodoma wakielekea uwanja wa Jamhuri yalikofanyika Maadhimisho ya Mei Mosi kimkoa. Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Jumanne Sagini (Mb) ndiye aliyeyapokea matembezi hayo kama Mgeni Rasmi.

Kitaifa Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani mwaka 2023 yalifanyika uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ndiye aliyekuwa Mgeni Rasmi.

Watumishi wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Ofisi ya Zanzibar na Ofisi za Matawi ya Dar es Salaam, Mwanza, Pemba na Lindi waliungana na wafanyakazi wengine katika kuadhimisha siku hiyo katika maeneo yao.