ADEM Logo
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA

Tunajenga utamaduni wa kuheshimu haki za binadamu, misingi ya utawala bora na utu wa mtu
ADEM Logo

THBUB YATOA MSAADA WA MAHITAJI MUHIMU KATIKA KITUO CHA ALHAAFIDHU ,KONDOA

09 Mar, 2023
THBUB YATOA MSAADA WA MAHITAJI MUHIMU KATIKA KITUO CHA ALHAAFIDHU ,KONDOA

 

Katika kuadhimisha Siku ya Wanawake DunianiWafanya kazi Wanawake  wa Tume ya Haki za Binadamu  na Utawala Bora   wametoa msaada wa mahitaji muhimu katika Kituo cha Alhaafidhu Islamic Center kilichopo Wilayani Kondoa,Mkoani Dodoma ,Machi 7,2023.

Akizungumza wakati wa kukabidhi msaada huo Kamishna wa Tume  ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Mhe.Amina Ali Talib alisema kuwa  kila Mwaka Tume inaadhimisha kwakugusa jamii kwakuwakumbuka wenye uhitaji kwakutoa msaada.

“Maadhisho ya Mwaka huu tumeona tutembelee kituo  hichi cha kulelea watoto  kutoa msaada ambao tunaamini  utawasaidia’’.Alisema Mhe.Amina

Aidha Bi.Amina alitoa wito kwa wanawake na watu mbalimbali kuwa na utaratibu wa  kutenga kiasi kwenye kile wanachopata  ili kusaidia jamii inayawazunguka hususani  watu kwenye makundi mahsusi kama yatima,wajane na watoto wa mtaani.

Kwa upande wake Bi.Aisha Khalfani  Nobbe ametoa shukrani kwa Uongozi wa Tume kwakutoa msaada  katika kituo hicho,kwani uhitaji ni mkubwa na kuwataka waendelee kusaidia makundi mengine yenye uhitaji.