ADEM Logo
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA

Tunajenga utamaduni wa kuheshimu haki za binadamu, misingi ya utawala bora na utu wa mtu
ADEM Logo

THBUB yapamba maadhimisho ya siku ya Wanawake 2024

10 Mar, 2024
THBUB yapamba maadhimisho ya siku ya Wanawake 2024

Leo Machi 8, 2024 Watumishi Wanawake wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora wameungana na wanawake wenzao nchini kote kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Wanawake iliyobeba Kauli mbiu isemayo: “Wekeza kwa Wanawake kuharakisha maendeleo ya Taifa na ustawi wa jamii.”

Hakika ushiriki wao uliifanya siku hiyo kuwa ya kupendeza kutokana na mavazi mazuri na ya aina yake waliyovaa. Itoshe kusema, ‘pamba’ walizopiga zilivutia macho ya kila aliyewatazama – walipendeza!

Kamishna wa THBUB na Msimamizi wa masuala ya Makundi Maalum, Mhe. Amina Talib Ali aliwaongoza Wanawake hao katika maadhimisho hayo mkoani Dodoma, ambako kimkoa yalifanyika viwanja vya Shule ya Msingi Chinangali wilayani Chamwino.

Uwepo wa THBUB pia ulionekana katika maadhimisho yaliyofanyika katika majiji ya Dar es Salaam na Mwanza ambako Tume inazo Ofisi zake za matawi.

Hii ni mara ya 27 Taifa letu linaadhimisha Siku ya Kimataifa ya Wanawake iliyoridhiwa na Umoja wa Mataifa na kuanza kuadhimishwa kwingine duniani mwaka 1975.