ADEM Logo
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA

Tunajenga utamaduni wa kuheshimu haki za binadamu, misingi ya utawala bora na utu wa mtu
ADEM Logo

Tanzania yapongezwa kwa kuweka miundominu wezeshi kwa walemavu

27 Oct, 2023
Tanzania yapongezwa kwa kuweka miundominu wezeshi kwa walemavu

Serikali ya Tanzania imepongezwa kwa kuendelea kusimamia haki za binadamu kwa makundi maalum ya  wazee na watu wenye ulemavu kwa kuweka miundombinu wezeshi ya kuwapunguzia adha mbalimbali ikiwemo matumizi ya lugha ya alama kwenye mikutano

Pongezi hizo zimetolewa leo tarehe 26 Oktoba 2024 wakati wa uwasilishwaji agenda kuhusu Utekelezaji wa Haki za Binadamu kwa Makundi Maalum ya Wazee na Watu wenye Ulemavu kwenye Kikao cha 77 cha Tume ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu kinachoendelea jijini Arusha.

Akizungumza kuhusu nafasi  ya Tanzania katika kusimamia haki za binadamu kwa makundi maalum ya wazee na wenye ulemavu, Mkurgenzi Msaidizi wa Idara ya Haki za Binadamu kutoka Wizara ya Katiba na Sheria, Bw. Richard Kilanga amesema kuwa Serikali imepiga hatua katika kuhakikisha makundi haya maalum ya watu wanapata haki zao za msingi kama wananchi wengine ikiwemo

chakula, malazi na mavazi.

Amesema kutokana na kuthamini mchango wa wazee  na watu wenye ulemavu kwenye maendeleo ya  nchi Ibara ya 11 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo inaelekeza mamlaka ya nchi kuweka utaratibu wa kuwawezesha kupata elimu na msaada kutoka kwa jamii wakati wa uzee, maradhi  au hali ya ulemavu na katika hali nyinginezo za mtu kama hajiwezi.

Ameongeza kusema katika kutekeleza jukumu la kusimamia kikamilifu ulinzi wa haki za binadamu kwa makundi  ya wazee

na walemavu, mwaka 2004 ilianzishawa Sera ya Watu wenye Ulemavu kwa upande wa Tanzania Bara na Sera ya aina hiyo ilianziswha Zanzibar mwaka 2018. Sera hizi zimeainisha namna watu wenye ulemavu wanavyopata huduma za elimu jumuishi, kazi, ajira na huduma za utangamano.

Pamoja na kuwepo kwa Sera hizo Serikali zote zimeweka Sheria ya Utekelezaji wa Sera hizo  mwaka 2010 kwa Tanzania Bara na mwaka 2022 kwa upande wa Zanzibar. Sheria hizi pamoja na mambo mengine zinaweka misingi muhimu kuhakikisha haki za watu wenye ulemavu zinahifadhiwa na kulindwa ikiwa ni pamoja na kuheshimu utu wa mtu, uhuru wa mtu kufanya maamuzi, kutobaguliwa

na kushiriki katika masuala yote ya kijamii, kupata taarifa, kuzingatia usawa wa wanawake na waaume na mahitaji yao na upatikanaji wa kiwango cha maisha yanayotakiwa na hifadhi ya jamii.

Pia mabaraza ya taifa kuhusu watu wenye ulemavu pamoja na Idara maalum kushughulikia masuala ya watu wenye ulemavu yameanzishwa Tanzania Bara na Zanzibar.

Kuhusu Wazee. Bw. Kilanga amekieleza kikao hicho kuwa, Serikali ya Tanzania imeendelea kuwatambua na kutoa huduma za msingi za chakula, malazi, mavazi na matibabu kwa wazee

wasiojiweza na watu wasiokuwa na watu wa kuwahudumia katika makazi 14 kwa upande wa Tanzania Bara.

“Zaidi ya wazee milioni mbili wametambuliwa katika mikoa 26. Kati ya wazee hao wanawake ni 735,169 na wanaume ni 1,382,468 kati ya wazee 586,772 sawasawa na asilimia 27 wamepatiwa vitambulisho vya bima ya afya kwa ajili ya matibabu ambapo wanawake ni  331,103 na wanaume ni 255,669,” alifafanua Bw. Kilanga.

Kikao cha Kawaida cha 77 cha Tume ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu kilifunguliwa rasmi jijini Arusha tarehe

20 Oktoba 2023 na kinatarajiwa kumalizika tarehe 09 Novemba, 2023. Pamoja na mambo mengine kikao kinapokea na kujadili agenda mbalimbali zinazohusu haki za binadamu katika nyanja za kiuchumi, kijamii na kisiasa.