ADEM Logo
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA

Tunajenga utamaduni wa kuheshimu haki za binadamu, misingi ya utawala bora na utu wa mtu
ADEM Logo

Mashirika yasiyo ya kiserikali ya IGT na BASIS yatembelea Tume

14 Mar, 2024
Mashirika yasiyo ya kiserikali ya IGT na BASIS yatembelea Tume

Mashirika mawili yasiyo ya kiserikali yanayojishughulisha na ukuzaji wa uwajibikaji,kwa pamoja leo Machi 12, 2024 yametembelea Makao Makuu ya Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB)jijiniDodoma na kufanya mazungumzo na uongozi wa juu wa Tume.

Katika mazungumzo yao, Tume na mashirika hayo mawili, BASIS International Limited la nchini Uganda na Shirika la Kukuza Utawala Bora na Uwazi Tanzania (Intiative for Good Governance and Transparance – IGT)lenye makao yake jijini Mwanza wametafakari kuhusu kuwa na mashirikiano katika ukuzaji na ulinzi wa haki za binadamu katika jamii zilizopo pembezoni mwa maeneo zinakofanyika shughuli za migodi.

Akiongea wakati wa mazungumzo hayo, Kamishna wa THBUB, Dkt. Thomas Masanja aliueleza ugeni huo kuwa Tume imefurahishwa na ujio wao,na kwamba taasisi yake iko tayari kufanya nao kazi.

Mkurugenzi wa IGT, Bwana Edwin Soko aliongoza Ujumbe wa taasisi hizo katika ziara hiyo akiambatana na maafisa wake wawili, Bi. Frida Mwenda (Afisa Programu) na Bi. Catherine Masanja (Afisa wa masuala ya Jinsia).

Wengine katika Ujumbe huo kutoka BASISInternational Limited walikuwa Bwana Tony Binyina(Meneja Miradi)na Bwana Michael Moasa(Meneja TEHAMA).