15
Fri, Jan
2 New Articles

Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora inafurahi kuwasilisha Mpango Kazi wa Kitaifa wa Haki za Binadamu (MKKHB) wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Tangu kuundwa kwa Muungano, Serikali ya Tanzania imejizatiti kuhifadhi na kukuza haki za binadamu kama zinavyofafanuliwa na Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania ya mwaka 1977 (kama ilivyorekebishwa mara kwa mara), Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 (kama ilivyorekebishwa hadi mwaka 2010), Tamko la Ulimwengu la Haki za Binadamu la mwaka 1948, pamoja na mikataba mingine ya Kikanda na Kimataifa. Kwa kuzingatia hali hii Serikali imeunda taasisi na vyombo mbalimbali kwa ajili kulinda na kukuza haki za binadamu, ikiwa ni pamoja na Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) lakini hakukuwa na mpango kazi maalum unaotekelezwa na vyombo vyote unaohusu haki za binadamu. Mpango huu uitwao MKKHB sasa unaweka msingi na mpangilio wa mambo ya kutekeleza. Mpango unadhihirisha azma ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya kutekeleza wajibu wake kimataifa na shauku ya Serikali katika kuboresha, kuhifadhi na kutekeleza haki za binadamu nchini. 

Sign up via our free email subscription service to receive notifications when new information is available.