04
Tue, Aug
3 New Articles

MAADHIMISHO YA SIKU YA MWANAMKE DUNIANI

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Press Release
Typography

 Tunapoadhimisha kumbukumbu ya siku ya Mwanamke Duniani  hii leo Machi 8, 2020 ikiwa ni miaka 25 tangu wanawake kutoka nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa wakutane jijini Beijing, China kujadili maendeleo ya wanawake,Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) inapenda kuungana na Watanzania wote katika kusherehekea maadhimisho haya ambayo kimsingi yanatoa fursa kwa wanawake kufanya marejeo ya hatua mbalimbali zilizofikiwa katika kuboresha mustakabali wa wanawake nchini.

Tume inatambua kuwa, Tanzania kama nchi mwanachama wa Umoja wa Mataifa imeridhia mikataba ya haki za binadamu kuhusu wanawake ikiwemo makubaliano yaliyofikiwa katika mkutano wa Beijing mwaka 1995. Soma zaidi

 

Sign up via our free email subscription service to receive notifications when new information is available.